Taasisi ya chakula na lishe inachelewesha mishahara


M

maluluma

Member
Joined
Mar 11, 2012
Messages
17
Likes
0
Points
0
M

maluluma

Member
Joined Mar 11, 2012
17 0 0
Ucheleweshaji wa mishahara ya wafanyakazi wa Taasisi ya Chakula na Lishe ni kubwa sana. Tatizo hili ni kubwa na ni la muda mrefu. Hili Janga kubwa. Uongozi wa taasisi umebadilika lakini tatizo hili halija pata ufumbuzi kabisa. Katika vikao malalamiko ya mishahara kuchelewa ni moja ya kero zinazo lalamikiwa lakini hakuna lolote. Mishahara tunapata kuanzania tarehe 3 au 4 ya mwezi mwingine na baada ya wafanyakazi kutabika sana. Mwezi bado hatujapata hakuna taarifa yoyote. Baada ya kuchelewa mfululizo katika mkutano wa wafanyakazi mwezi wa kumi wafanyakazi walilalamika. Mhasibu Mkuu mpya aliahidi kutatua na mwezi wa kumi mishahara iliwahi lakini mwezi tena hali imerudi imechelewa zaidi. Majibu mengi ya malalmiko nikwamaba cheki ya mshahara ina chelewa kuletwa hapa taasisi. Je, wizara ya afya na hazina wanachelewesha cheki za mishahara wakati serikaliilisha tangaza kuwa wafanyakazi wapate mishahara tarehe 25.

Lakini taasisi tatizo kubwa ni uongozi ambao haujali wafanyakazi wadogo kwakuwa viongozi wengi wana mishahara mikubwa, marupurupu mengi. posho nyingi, safari nyingi. wanapata fedha kila siku iendayo kwa mungu. Ndio maana hawajali maslahi wa wafanyakazi wadogo. Mfanyakazi mwenye mshahara lakimbili au tatu na hana marupupu yoyote yale na abnategemea asafiri kwenda na kurudi kazini gari zaidi ya moja na akodi bodaboda, ale na familia yake, awape watotokwenda shule, alipe kodi ya nyumba na mshahara huo unachelewa zaidi ya mwezi ataishi vipi. Huruma inatakiwa hapa.

Taasisi hii huko nyuma ilikuwa ya mfano chini ya uongozi wa kavishe. Alikuwa na mipango yakimaendeleo sana. Alijenga nyumba za wafanyakazi, aliweka viwanja kwaajili ya wafanyakazi, alinunua magari na alijali sana wafanyakazi na wananchi . Leo hii taasisi haina viwanja hata kimoja huko kunduchi vyote wamegawana wakubwa, nyumba zimechakaa, majengo ya taasisi yamechakaa, magari yamechaka na sasa hata mshahara unachelewa. Hakuna anayejali mfnayakazi. Kila kiongozi wa taasissi anajali maslahi yake binafsi. Sisi wafanyakazi tunaomba mamlaka husika ofisi ya wazirimkuu, wizaya afya na ustawi wa jamii na bodi washughulike na suala la uongozi ni bora atafutwe kiongozi kutoka nje ya wafanyakazi / taasisi ili kuvunja mwiko wa utamaduni wa kulindana, kutojali wafanyakazi na kujali maslahi binafsi badal ya umma
 

Forum statistics

Threads 1,251,973
Members 481,948
Posts 29,791,976