Taarifa ya Mkanganyiko na kutohusika na Utapeli wa ajira kwa vijana-YAP Tanzania

Mvumbagu

Member
Nov 30, 2013
38
0
Angalizo: Uki search kwenye google utakutakuta kuna 1. Watoto wetu Tanzania-Youth awareness program(YAP) 2. Youth Awareness Program Tanzania (YAP-Tanzania).

1.) Watoto wetu Tanzania - Youth Awareness Program (YAP), hii iko Kimara suka mkabala na kanisa katoliki Mavurunza, na ni kwa ajili ya Watoto yatima na vijana wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi tu ndani ya kituo cha Watoto wetu Tanzania pekee, na ambapo kwa sasa program hii imesimama kwa muda-karibu mwaka mmoja sasa.

watu wengi wamekuwa wakiwasiliana na kituo hiki kupitia contacts zao zilizopo kwenye tovuti yake ya www.wwtz.org pamoja na facebook page yao www.facebook.com/yaptz

NB: Watoto wetu Tanzania - Youth Awareness Program (WWT-YAP) Hii haina na haitambui uwepo wa Program za nje kama hizo za kulipia na haitoi ajira

2. Youth Awareness program Tanzania (YAP TANZANIA), ambayo inasema kuwa iko zanzibar na kushirikiana na Graduate International hii ndio ya hao matapeli..wanasema wanatoa nafasi za ajira 70 na kuchaji pesa 30,000/- kwa ajili ya training ili upate ajira ya awareness officers nk.

Guys, Hawa jamaa wa pili ni Matapeli, Usithubutu kuwatumia pesa zako. Kazi gani hadi utoe pesa...TAHADHARI NA HAWA MATAPELI- Ikiwezekana wawe traced na kukamatwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom