viatu virefu
Senior Member
- May 25, 2015
- 165
- 20
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA UMEME KWA BAADHI YA MAENEO YA MKOA WA ILALA KUTOKANA NA KUUNGUA KWA VIKATA UMEME KWENYE KITUO CHA GONGOLAMBOTO.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Ilala Wilaya ya Gongolamboto kuwa usiku wa kuamkia leo Februari 21,2016 imetokea hitilafu ya kuungua kwa vifaa vya kukata umeme "Circuit Breakers" kwenye Kituo chetu cha kupooza na kusambaza umeme cha Gongolamboto na hivyo kusababisha maeneo ya GONGOLAMBOTO, KISARAWE, ULONGONI, MONGOLANDEGE, MOSHI BAR na maeneo yote ya jirani kukosa umeme. Kama tulivyowajulisha awali mafundi walianza kazi usiku na zoezi la kubadilisha vifaa hivyo linaendelea. Tunatarajia umeme utarudi jioni ya leo au usiku wa leo baada ya kazi hiyo kukamilika.
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu.