Taarifa ya kukatika kwa Umeme Mkoani Dodoma

hakuna shida

Member
Dec 16, 2015
25
5
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)


TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA UMEME MKOANI DODOMA.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wa Mkoa wa Dodoma kuwa kumetokea hitilafu katika Transfoma kubwa inayosambaza Umeme katika mkoa huo na kupelekea Dodoma mjini na baadhi ya wilaya zake kukosa Umeme tangu saa 3.15 asubuhi ya leo 24/12/2015.

Mafundi wetu wapo tayari katika mtambo huo kubaini chanzo cha tatizo hilo. Tutawapa taarifa pindi matengenezo yatapokamilika na Umeme kurudi katika hali ya kawaida.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utaojitokeza.

Imetolewa na; Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu.
 
ahsante umesharudi

Labda kwako mimi sina umeme tangu saa mbili asubuhi na haujarudi, kwanza wanafiki iweje leo watufahamishe mbona wanavyokata siku zingine hawatufahamishi? Hili shirika sio jipu ni tambazi kutumbuliwa kwake kunahitaji jambia sio pini wala wembe
 
Back
Top Bottom