Taarifa ya hali ya upatikanaji wa umeme kwa baadhi ya maeneo ya mikoa jioni hii

hakuna shida

Member
Dec 16, 2015
25
5
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA HALI YA UPATIKANAJI WA UMEME KWA BAADHI YA MAENEO YA MIKOA JIONI HII.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kuwataarifu wateja wake wa baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kinondoni Kusini, Kinondoni Kaskazini na Mkoa wa Mwanza kuwa umeme umekatika kwa sababu zifuatazo:-

K'KUSINI:
Line ya Nordic imetoka ghafla majira ya saa 12 jioni hii Januari 21, 2016 na mafundi wamegundua kuwa kuna waya zimekatika eneo la Baruti. Maeneo yanayokosa umeme ni Baruti, Kimara, Korogwe, Mbezi Temboni, Mbezi Luis, Luguruni,Matosa na Kibamba. Umeme utarejea muda mfupi ujao.

K'KASKAZINI:
Kwenye Kituo cha kusambaza umeme cha Mikocheni ambacho jana Jan 20, kiliingiliwa na maji kutoka na mvua nyingi kimezima tena baada ya mafundi kurudisha umeme jana. Jioni hii umetokea mlipuko na hivyo maeneo ya
Mikocheni kwa Warioba, kwa Nyerere na Maeneo ya viwandani yatakosa umeme mpaka kesho. Mafundi wapo site kubadili kifaa kilichoungua.

MKOA WA MWANZA
Njia ya kupeleka umeme Wilaya ya Sengerema imetoka jioni hii na mafundi wanafuatilia tatizo. Maeneo yanayokosa umeme ni Geita mjini, wilaya ya Sengerema, Sayona steel mills na baadhi ya maeneo ya mkoa Mwanza.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza na Tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu
 
Back
Top Bottom