Taarifa ya Bodi ya Utalii Nchini Kupinga Taarifa Zinazosamba Kuhusu Olduvai

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imekuwa ikifuatilia kwa makini majadiliano yanayoendelea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kufuatia video iliyotumwa katika YouTube
na imekuwa ikisambazwa kupitia njia mbalimbali za habari ikimuonesha mtu mmoja kutoka nchi jirani akisema kuwa Olduvai Gorge ambayo kimsingi iko Tanzania kwamba iko Kenya.

Video hii imeibua majadiliano katika mitandao ya kijamii baina ya watanzania na watu wengine ambao wanaitakia mema Tanzania na wanaoelewa vizuri kuwa Olduvai Gorge iko Tanzania.

Bodi ya Utalii Tanzania kama taasisi ya Umma yenye jukumu la kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii imeshtushwa na video hii iliyojaa upotoshwaji mkubwa ambao tunaamini mbali ya malengo mengine inalenga kuchafua kazi nzuri ambayo imekuwa ikifanywa na Bodi kwa kushirikiana na wadau wengine katika kutamgaza vivutio vya utalii vya Tanzania ikiwemo Olduvai Gorge.

Tunapenda kuchukua fursa hii kupinga vikali upotoshwaji huu uliofanywa na mtu huyo wakati akihutubia mkutano ambao tumeambiwa ulikuwa ni wa Vijana wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Amerika mwezi Agosti mwaka jana.

Tunapenda dunia ifahamu kuwa kama ilivyo kwa Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Zanzibar n.k Olduvai Gorge mahali panapoaminika kuwa ndipo binadamu wa kwanza duniani aliishi na ambako Dr. Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la binadamu huyo wa kale anayesadikiwa kuishi miaka takribani milioni 2 iliyopita iko pia Tanzania na si mahali pengine popote duniani. Eneo hili la Olduvai Gorge liko katika bonde la ufa katikati ya bonde la Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Manyara nchini Tanzania.

Tunatoa wito kwa watanzania mahali popote walipo kuendelea kuunga mkono juhudi za Bodi ya Utalii Tanzania za kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya Utalii kwa kujibu na kusahihisha papo hapo bila woga mara tu taarifa ya upotoshaji kuhusu nchi yetu inapotolewa iwe ni kwenye mikutano ya ndani ya nchi au ya Kimataifa.

Tunaamini kuwa ni jukumu la kila mtanzania kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya Utalii badala ya kuiachia TTB kazi hii peke yake.

Yawezekana katika mkutano huo wa vijana ambao mjumbe huyo wa nchi jirani alipata fursa ya kuzungumza na kufanya upotoshaji huzo, wajumbe wa Tanzania pia walikuwepo ambao wangweza kukosoa upotoshaji huo papo hapo na kuelezea ukweli na usahihi wa mahali ilipo Olduvai Gorge.

Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano

BODI YA UTALII TANZANIA
 
Hivi Ngorongoro ipo Manyara au Arusha?wakenya wapo sahihi kama hata vya kwetu tunakosea.Tunaomba mkuu wa mkoa wa Arusha apinge huu upotoshaji..
 
Tujuze kama kweli wajumbe toka Tz walikuwepo, ni akina nani na kwa nini hawakusahihisha upotoshaji huo. Hawawezi kuongea kizungu?
 
Ukweli ni kwamba TTB mmejikalia tu. Hamfanyi kazi ipasavyo,iweje video iwepo tangu mwaka Jana Agost lakini mpk leo March hamjajua bado? Mpo wapi?
Then badala ya kutoa sahihisho kwamba mtafanya nn katika kuikanusha taarifa hiyo iliyopotosha sehemu kubwa ya dunia,eti mnakuja kusema tuendelee kuwasapoti.
Nyie pia ni Jipu. Nothing new
 
Kumbe na sisi watanzania ni wakenya :D :D
ImageUploadedByJamiiForums1456772483.190182.jpg
 
'' Bodi ya Utalii Tanzania kama taasisi ya Umma yenye jukumu la kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii imeshtushwa na video hii iliyojaa upotoshwaji mkubwa ambao tunaamini mbali ya malengo mengine inalenga kuchafua kazi nzuri ambayo imekuwa ikifanywa na Bodi kwa kushirikiana na wadau wengine katika kutamgaza vivutio vya utalii vya Tanzania ikiwemo Olduvai Gorge...............
Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano

BODI YA UTALII TANZANIA''

N.B

ANGALIZO KWA BODI YA UTALII

Bodi ya Utalii Tanzania msifanye kazi kwa ''mizuka'' kaeni chini mtoe TAMKO pia kwa lugha fasaha ya Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa, Kispaniola, Kiarabu, KICHINA, KIJAPANI. Haya mambo ya kukimbilia kutoa tamko kwa lugha ya Kiswahili pekee haitoshi mrudi tena hapa tuone kazi yenu ya kutetea vivutio hivyo adhimu duniani vinavopatikana Tanzania kwa lugha hizo taja za kimataifa.

Pia tunataka kuona kitu cha nguvu a.k.a video clip ya quality ya kimataifa kama matangazo mengine ya makampuni makubwa katika YOUTUBE kwa lugha hizo kikinadi vivutio vya Utalii Tanzania. Ikiwezekana kopi mtuletee hapa JamiiForums tuifanyie vetting maana Jamiiforums ina wadau kila kona ya dunia na hivyo kuweza kupendekeza au kutoa mawaidha namna ya kufahamisha dunia vivutio vyetu vya utalii.
''
 
TATIZO LA KUPEANA KWA KUJUANA NAFASI ZA UWAKILISHI WA MIKUTANO MIKUBWA NA MAENEO NYETI LIMEIGHARIMU SANANTANZANIA.
INAWEZEKANA WALIOKUWEPO KTUWAKILISHA HAWAJUI KUANDIKA WALA KUONGEA KIINGEREZA KWA UFASAHA NA HIVYO KUSHINDWA KUIKOSOA KAULI HIYO YA MKENYA HADHARANI.
ATAFUTWE/WATAFUTWE WALIOTUWAKILISHA TUWAHOJI KWA KUWA KWAO KIMYA NI KUTOJUA HISTORIA YA NCHI YAO YENYE MITO NA MABONDE MENGI YA NAFAKA AU NI KUKOSA UZALENDO?
 
Ha ha mnakanuashia kwenye JF na social media zingne alafu kwa kiswahili,nendeni mkakanushie a NEW YORK TIMES,CNN ALJAZEERA NK tena kwa lugha zote kubwa duniani
 
Huyo Olduvai George, Mlima Kilimanjaro, Tanzanite, Serengeti, Ngorongoro wamenisaidia nini katika kuboresha maisha yangu na watanzania wengine maskini mpaka leo?!!

Wawachukue tu, wananihuzunisha nikiwatazama; Siwahitaji.
 
TATIZO LA KUPEANA KWA KUJUANA NAFASI ZA UWAKILISHI WA MIKUTANO MIKUBWA NA MAENEO NYETI LIMEIGHARIMU SANANTANZANIA.
INAWEZEKANA WALIOKUWEPO KTUWAKILISHA HAWAJUI KUANDIKA WALA KUONGEA KIINGEREZA KWA UFASAHA NA HIVYO KUSHINDWA KUIKOSOA KAULI HIYO YA MKENYA HADHARANI.
ATAFUTWE/WATAFUTWE WALIOTUWAKILISHA TUWAHOJI KWA KUWA KWAO KIMYA NI KUTOJUA HISTORIA YA NCHI YAO YENYE MITO NA MABONDE MENGI YA NAFAKA AU NI KUKOSA UZALENDO?
Wakishajulikana hao watz waliokuwepo siku hiyo wapigwe viboko hadharani!haiwezekani mtu anadanganya na mpo tu mnachekelea na kupiga makofi..Bodi nayo ni jipu,tukio la mwaka jana wanatoa tamko leo..nao viboko!
 
Halafu nawaomba wana-JamiiForums tunapokuwa tunachangia ''comments'' katika mitandao ya kijamii-kimataifa , youtube , news google , Yahoo News, magazeti ya kimataifa, intaneti tuwe tunatumia jina la nchi yetu kikamilifu badala ya kuandika kwa kifupi TZ tuwe tunaandika TANZANIA.

Wenzetu Kenya,Nigeria, Zimbabwe n.k ukiona mtu anatoa comments ktk youtube kuhusu DiamondPlatnumz, King Ali Kiba, Ruby Milima ya Kwetu utakuta mtu anamalizia au kuelezea kwa kutumia KENYA, NIGERIA n.k , hivyo tutumie fursa hizo tutumie jina rasmi TANZANIA badala ya kifupisho TZ.
 
BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imekuwa ikifuatilia kwa makini majadiliano yanayoendelea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kufuatia video iliyotumwa katika YouTube
na imekuwa ikisambazwa kupitia njia mbalimbali za habari ikimuonesha mtu mmoja kutoka nchi jirani akisema kuwa Olduvai Gorge ambayo kimsingi iko Tanzania kwamba iko Kenya.

Video hii imeibua majadiliano katika mitandao ya kijamii baina ya watanzania na watu wengine ambao wanaitakia mema Tanzania na wanaoelewa vizuri kuwa Olduvai Gorge iko Tanzania.

Bodi ya Utalii Tanzania kama taasisi ya Umma yenye jukumu la kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii imeshtushwa na video hii iliyojaa upotoshwaji mkubwa ambao tunaamini mbali ya malengo mengine inalenga kuchafua kazi nzuri ambayo imekuwa ikifanywa na Bodi kwa kushirikiana na wadau wengine katika kutamgaza vivutio vya utalii vya Tanzania ikiwemo Olduvai Gorge.

Tunapenda kuchukua fursa hii kupinga vikali upotoshwaji huu uliofanywa na mtu huyo wakati akihutubia mkutano ambao tumeambiwa ulikuwa ni wa Vijana wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Amerika mwezi Agosti mwaka jana.

Tunapenda dunia ifahamu kuwa kama ilivyo kwa Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Zanzibar n.k Olduvai Gorge mahali panapoaminika kuwa ndipo binadamu wa kwanza duniani aliishi na ambako Dr. Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la binadamu huyo wa kale anayesadikiwa kuishi miaka takribani milioni 2 iliyopita iko pia Tanzania na si mahali pengine popote duniani. Eneo hili la Olduvai Gorge liko katika bonde la ufa katikati ya bonde la Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Manyara nchini Tanzania.

Tunatoa wito kwa watanzania mahali popote walipo kuendelea kuunga mkono juhudi za Bodi ya Utalii Tanzania za kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya Utalii kwa kujibu na kusahihisha papo hapo bila woga mara tu taarifa ya upotoshaji kuhusu nchi yetu inapotolewa iwe ni kwenye mikutano ya ndani ya nchi au ya Kimataifa.

Tunaamini kuwa ni jukumu la kila mtanzania kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya Utalii badala ya kuiachia TTB kazi hii peke yake.

Yawezekana katika mkutano huo wa vijana ambao mjumbe huyo wa nchi jirani alipata fursa ya kuzungumza na kufanya upotoshaji huzo, wajumbe wa Tanzania pia walikuwepo ambao wangweza kukosoa upotoshaji huo papo hapo na kuelezea ukweli na usahihi wa mahali ilipo Olduvai Gorge.

Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano

BODI YA UTALII TANZANIA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom