barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,865
TAARIFA POTOFU KUHUSU WAFADHILI 10 KUSITISHA MISAADA YAO KWA TANZANIA
Kumekuwapo taarifa potofu kwamba Wahisani karibu 10 wamesitisha misaada yao kwa Serikali ya Tanzania. Taarifa hizi ni za uongo na upotoshwaji na zinalenga kuleta taharuki miongoni mwa jamii ya watanzania.
Binafsi kama raia ili kujiridhisha nimewasiliana na Wizara ya Fedha na balozi mbili (kupitia Maafisa wao waandamizi) na kote taarifa hizi hazina ukweli wowote.
Kilichotokea ni Mwandishi wa Shirika moja la Habari la nje, kunukuu vibaya mazungumzo ya kiongozi wa Wizara ya fedha wakati wa shughuli ya kutiliana saini msaada uliotolewa na Serikali ya Japani kwa Tanzania.
Kilichotakiwa kuripotiwa ni kwamba, wafadhili hapa Tanzania wanaisaidia Serikali kwa njia mbalimbali ikiwemo (a) Mfuko wa Pamoja wa kusaidia bajeti ya Serikali au "General Budget Support (GBS) (b) Misaada ya Kisekta kama vile kilimo, nishati na usafirishaji pamoja na (c) Misaada kwa miradi.
Kilichotokea ni kwamba nchi wahisani sera zao zimekuwa zikibadilika kipindi hadi kipindi na kupelekea kubadilika kwa mtindo wa kutoa msaada kwa nchi yetu. Nchi kadhaa zimeonelea zisiendelee kusaidia Tanzania kwa mtindo wa GBS na badala yake wanaendelea kusaidia Tanzania katika sekta na miradi husika. Sekta hizi na Miradi hii iko katika vipaumbele vya Serikali.
Mwandishi yule wa Habari alijikanganya na kuchanganya maelezo hayo juu na kujulisha chombo chake cha Habari na hatimaye umma wa watanzania taarifa ambazo sio za kweli.
Rai yangu kwa Wananchi wenzangu, ni kwamba ni kweli misaada ni jambo jema lakini ni bora isije kama itakuwa inakuja katika masharti yanayotweza utu na heshima ya Taifa letu Tanzania.
Humphrey Polepole
Raia wa Tanzania
NB: KESHO ASUBUHI IJUMAA TAREHE 1 NITAKUWA CHANNEL 10 KUENDELEA NA UCHAMBUZI NA UFAFANUZI WA MASUALA HAYA.