mwadu boy
Member
- Oct 10, 2021
- 53
- 28
Salaam zenu na kongole nyingi kwa wana nasaba ya Afrika.
Ni mimi mzalendo
Taarifa yangu inalenga shabaha kwa VIJANA wa Kitanzania. Nimesoma vijarida vingi vidogovidogo vya Shujaaz mwandishi akiwa Dj Tee nikaona mambo mengi sana kuhusu vijana ingawa bado kuna mambo mengi vijana hawayajui walau kijarida hiki ni muhimu kwa jamii.
Badala ya kutangatanga mitandaoni kwanini tusimfuatilie huyu kijana walau tukapata KAZI nzuri mitaani na kujitafutia maarifa kijarida hiki ni kijiwe kipya cha vijana badala ya kuhangaika club kunywa bia na kufanya uzinifu wa hisia na macho. Hatuendelei kwa sababu hatuchanganyi akili zetu na maarifa.
Asilimia kubwa ya vijana wamefocus kwenye starehe badala ya KAZI zao. Jaribu kufikiria umetumia Mda gani kufanya biashara yako kuwa ya kipekee, kujifunza kilimo, kujaribu mbinu mpya kwenye chochote unachofanya, umeboreshaje huduma yako. Kiukweli huna huo Mda! Nini mnachokisikia masikioni mechi za Ulaya na soka la watani wa jadi. Au ngoma mpya ya konde au simba. Au kuhusu mademu mlioruka nao disco jana. Mlivyolewa jana kwenye baa au vichekesho kweli maisha yenu yamejaa sanaa na bata ambalo bata linashangaa
Sanaa inatuburudisha kweli kweli . Ila kweli inakunufaisha wewe au wewe unainufaisha sanaa. Acha kufuatilia vitu visivyo na maana maishani kwako. Fanyeni mazoezi, boresheni KAZI za mikono yenu siku kwa siku, punguzeni Udhaifu wenu kwa kutafuta maarifa na ujuzi. Usitukuze alama za wengine maishani. Ooooh mchezaji conc. Timu yetu kimayere mayere. Simba ndo baba lao. Alaaa!
Acha alama yako bora kabisa mtaa wote ukujue vijiji vikuone shujaa wao, watu wapende huduma yako au bidhaa zako.
Vijana chekecheni akili acheni kusikiliza siasa za viongozi uchwara.
Kwako SHUJAAZ umekuwa mtetezi lakini hujatimiza azma. Lazima uteke akili za vijana wengi kiasi cha kufanya serikali iache kuwaona maboya. Serikali inawatesa vijana mno kwa kutotambua kuwa wao ndo mchango mkubwa imewalevya vijana na siasa ooh mara CHAVITA mara UVICCM sioni umuhimu wa kuwaumiza vijana acheni vijana waishi maisha yao ya bila Uvyama tekelezeni wajibu wenu.
Shujaaz hujakata kiu ya Vijana bado!
Funzo acha kufuatilia starehe tafuta maarifa unayohitaji kukomboa familia yako na jamii yako kwenye umaskini. Tumia Mda mwingi kazini kwako ili maarifa yakufungukie ugundue na kubuni mbinu mpya na ujuzi wa siri kwenye fani yako ili umrithishe mwanao tu mkawa wa kipekee.
Nchi kwenu mmetudanganya mmkalia mamlaka kwa pesa za wanannchi za kodi KAZI zenu za kizembe.
Tunataka kiongozi chuma kama
MAGUFULI jembe. Sio siasa
Mwadu17. Toa Tamaa Udhaifu na Uovu nafsini kwako.