JUkonga
Member
- Dec 30, 2015
- 14
- 13
✅Leo tarehe 02.02.2016 ni Siku ya kusikilizwa kwa shauri no. 49 ya mwaka 2016, lililofunguliwa Mahakama kuu ya Tanzania Kitengo cha Ardhi na wakazi wa Kata za Ukonga, Gongolamboto na Pugu waliowekewewa X kwenye nyumba zao ili zibomolewe. Kama mnavyokumbuka shauri hili lilifunguliwa kwa msaada wa Mbunge wa Ukonga Mh Waitara Mwita kupinga utaratibu unaotumiwa na serikali kuwaondoa wakazi wa mabondeni. Katika Shauri hili wakazi wa bonde la mto msimbazi kwa maeneo ya Ukonga, Gmboto na Pugu wanawakilishwa na Wakili Msomi Dr. Onesmo Kyauke. Kwa mara ya kwanza shauri hili lilisikilizwa tarehe 21.01.2016 na mahakama ikatoa zuio la muda ili nyumba za wakazi hao zisibomolewe hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa.
✅Msimamo wa Mbunge wa Ukonga Mh. Waitara Mwita ambao ndiyo msimamo wa Wananchi kwenye sakata hili la wakazi wa mabondeni ni kuwa Serikali ifuate utaratibu wa kisheria kutatua matatizo haya ya Wakazi wa Mabondeni na kubwa ni wananchi wafidiwe nyumba ma mali zao na wapewe muda ili wahame kutoka mabondeni.
✅Kwakuwa wakazi hawa wa mabondeni wameuziwa maeneo hayo na wanamiliki huku serikali katika ngazi ya Mtaa, Kata inajua na ilishiriki kuhalalisha maeneo hayo na baadaye watu wakajenga na kuanza kuishi kwa muda mrefu wengine Zaidi ya miaka 10, serikali inatakiwa kuliona hilo kwa sababu siyo haki kuwavunjia watu nyumba zao na kuwaharibia mali zao kinyume na utaratibu. Serikali zilizopita ilipeleka huduma za jamii kama Maji, Umeme na Barabara kwenye maeneo mengi ya mabondeni jambo linalohalisha serikali kuwatambua watu hao wa Mabondeni.
✅Kuna maswala ya haki za Binadamu, wakazi hasa wa mabondeni wengine wana watoto wadogo, Wazee, Wagonjwa na wengine na mayatima, Walemavu na Wajane n.k ni lazima serikali ilinde haki za hawa watu.