Taarifa kwa Vyombo vya habari na Umma wa Tanzania.(Don Nalimison)

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,334
WARAKA WA WAZI KWA MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA, MKUU WA MKOA WA MWANZA NA KWA UMMA WA TANZANIA.

Nachukua fursa hii kuwajulisha kuwa Mimi DON NALIMISON ambaye zamani nilijulikana Kama DEOGRATIUS KISANDU kuwa Sasa Mimi sio tena MTUMISHI WA UMMA yaani sio tena MFANYAKAZI WA SERIKALI kutokana na unyama niliofanyiwa na Wilaya ya Nyamagana na Mkoa mzima wa Mwanza.

Nilifungwa miaka 3 tangu 2018 na nimemaliza kifungo gereza Kitengule tangu 26/6/2020 na Niko huru kiakili na kiafya. Sina UKIMWI, SINA UGONJWA WA AKILI Wala Mimi sio HANISI. Ni mtanzania mwenye mitazamo ya kimabadiliko.

Nilipo maliza kifungo nililipoti kazini lakini sikupokelewa kwa kuwa nilikuwa nimefungwa. Hivyo nimefanya yafuatayo:

1.Niliandika barua ya Kuacha Kazi kwenda kwa Mkurugenzi Jiji la Mwanza tangu july2020.

2.Nimekabidhi Kitambulisho Cha Kazi kwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza.

3.Nilirudisha Kitambulisho Cha NIDA ambacho ni batili na kumkabidhi Mkurugenzi Jiji la Mwanza kupitia masijala.

4.Nimerudisha pia Kitambulisho Cha CWT kupitia mwenyekiti wa tawi la Mkolani sekondari.

5.Nimenyimwa haki ya kupata Kitambulisho kipya Cha NIDA kwasababu za Kijinga.

6.Nimerudisha pia Kitambulisho Cha LAPF pale ofisi za PSSF na wakakipokea baada ya kugoma kunipa MAFAO yangu, hizo pesa kuleni na watoto wenu.

7.Pia Bayport wamenidhurumu Pesa zangu ambazo waliendelea kunikata ili Hali mkopo uliisha tangu septemba 2019. Hizo pesa nazo kuleni na watoto wenu.

8.Ualimu ni wito kwa wajinga wanaoonewa nakubaki kufanya kazi ya KUONEWA.

9.Sina MKE Wala Wake lakini Halmashauri imepandikiza Wanawake na kuwafanya wake zangu kwa mazingaombwe. Mimi sio fala kabisa.

10.Halmashauri imekuwa ikiingilia maisha yangu binafsi utafikiri ni mademu zangu na mahawala zangu, Ni ujinga kuingilia maisha ya mwajiriwa wakati sio ndugu yenu.Aidha wengine wamejipachika undugu ili kuniharibia.

11. Mishahara ulisimamishwa ili Hali sijawahi kupewa barua ya kufukuzwa kazi au kusimamishwa.

12.Nawatakia kazi njema na anguko la serikali yenu.

Wenu

DON NALIMISON.
5/9/2020
SimunNa. 0682 94 29 01.
DODOMA.
FB_IMG_1599309102157.jpg
 
Kama sio maigizo... basi ndugu yetu huyu.. .. akatembee dodoma na mapema kabla hakija ripuka!
 
Kama sio maigizo... basi ndugu yetu huyu.. .. akatembee dodoma na mapema kabla hakija ripuka!
Mzoe huyu tangu kitambo hapa tunamjua,wiki iliyo pita alionyesha nyaraka zinazo onesha kapimwa akili yupo good mentally health
 
Don unapiga kiswahili safi sana, umfundishe na yule jamaa yenu aliyetangaza ajira 13000 sababu tu ya kumuogopa Lissu
 
Hujawahi kuniangusha mwamba na siku zote hufanya nicheke nikisoma nyuzi zako Mwamba!
 
Back
Top Bottom