Taarifa kwa vyombo vya habari juu ya unyanyasaji na udhalilishwaji wa madaktari nchini

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
04/03/2017

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA UNYANYASAJI NA UDHALILISHWAJI WA MADAKTARI NCHINI.

Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) ni chama cha kitaaluma cha Madaktari wa binadamu kilicho anzishwa mwaka 1965 kwa madhumuni ya kuendeleza na kuwalea wanataaluma kimaadili na ueledi wa kitaaluma na kusimamia taaluma ya udaktari nchini Tanzania. Hivyo basi chama hiki kinajukumu la kuwasimamia kwa kushirikiana na Baraza la Madaktari Tanganyika katika kutoa huduma iliyotukuka kama inavyokusudiwa na jamii.

MAT na Madaktari kwa ujumla wamepokea kwa masikitiko matukio mbalimbali ya Madaktari na wafanyakazi wengine wa afya kunyanyaswa na viongozi mbalimbali nchini, ikiwemo kuwekawa ndani(lockup) kwa baadhi ya Waganga Wakuu wa Wilaya hapa nchini.

Imeonekana kama viongozi wengi hasa wakuu wa wilaya na mikoa wanatoa matamko ambayo kwa namna moja ni ya kuwadhalilisha madaktari na wahudumu wa afya, MAT ambacho ni chama kinachosimamia maadili na ueledi wa wanataaluma nchini TUNASIKITISWA SANA KWA VITENDO HIVI NA HATUTAKUBALINA NA UONEVU HUU HATA KIDOGO.

Tukio la lililosikitisha la hivi karibuni ni lile ya Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Bwana Christopher Emil Ngumbiagai ambapo mbele ya wafanyakazi na kamera za wandishi wa habari alimuamuru OCD kumuweka ndani (lock up) Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Dr. Vitalis Katalyeba, sababu ikiwa hakuwa na barua ya kusimamishwa kazi.

Ambapo kitaratibu inafahamika Mkurugenzi wa wilaya ndiye aliyepaswa kumpa Mkuu wa wilaya barua ya kumsimamisha kazi Daktari. Kwanini Daktari awekwe ndani kwa kosa lisilo lake, na kwanini isiwe Mkurugenzi ndio akamatwe na kuwekwa ndani?!!

Tukio lingine lilitokea Singida vijiji ambapo mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Rehema Nchimbi alimuweka ndani (lock up)_ Mganga Mkuu wa Wilaya ya Singida mjini Dr. Erick Bakuza. Pamoja na kuwa kulikuwa na mapungufu ya kiutendaji, haikuwa sahihi hata kidogo kumuweka lock up mganga mkuu wa wilaya ila taratibu za kinidhamu zilitakiwa kufuatwa.

Tukio la tatu linamhusu Mganga Mkuu wa a wilaya ya Monduli na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Mrisho Gambo ambaye alimtaka mganga mkuu wa wilaya ya Monduli kutoa maelezo ya juu ya malipo ya malimbikizo mbalimbali ya stahiki za watumishi wa afya pamoja ucheleweshwaji wa kupandishwa vyeo/madaraja kwa watumishi wa afya huku akijua siyo jukumu la mganga mkuu wa wilaya.

WITO

Udhalilisha huu USITISHWE mara moja nchi nzima.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Bwana Christopher Emil Ngumbiagai ajitathmini mwenyewe kabla hatujamchukulia hatua kwa udhalilishaji alioufanya. Tunawataka madaktari wote nchini kutompa ushirikiano Bwana Christopher Emil Ngumbiagai kwa sababu ni adui wa taaluma ya udaktari nchini na adui wa maendeleo ya afya wa watanzania.

Hatutavumilia tena uonevu na udhalilishaji wa madaktari kama huu, tutachukua hatua stahiki ya kulinda taaluma yetu ambayo inaheshimika ulimwenguni kote kwa manufaa ya umma.

Serikali itekeleze wajibu wake wa kulipa stahiki za watumishi wa afya pamoja na kuwapandisha vyeo/ madaraja watumishi wa afya na kuacha kuwasingizia waganga wakuu wa wilaya kwenye majukumu yasiyo yao pale inaposhindwa kutekeleza wajibu wake.

Tararatibu za kiutumishi na utawala zifuatwe pindi panapoonekana kuna changamoto katika utendaji au ufanyaji kazi katika sekta ya afya.
Pamoja na mambo mengine tunamtaka Waziri wa Afya maendeleo ya jamii, jinsi, wazee na watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu kuwasilisha Muswaada wa Madaktari, Madaktari wa Meno na wanataalamu shirikishi wa afya Bungeni kwenye Bunge lijalo hata ikibidi kwa hati ya dharula

Kwa kuwa muswada huo una manufaa makubwa ya kuilinda jamii inayohudumiwa na wataalamu wa afya. Pia Muswada huo utaleta dhana ya uwajibikaji na weledi kupitia elimu endelevu na kuboresha utoaji huduma za afya nchini. MAT pamoja na wadau wengine wa afya hatukubaliani na ucheleweshaji wa muswada huu.

MAT tunaiomba serikali kutoa kibali cha ajira kwa madaktari wenye sifa takribani 1794(elfu moja mia saba tisini na nne) ambao wapo mtaani bila ajira kwa kuzingatia uhitaji wa Mikoa hasa ile yenye uhaba mkubwa wa madaktari.

Katika kuzingatia uadilifu na huduma bora ya afya kutoka kwa Madaktari Tanzania, MAT tunaunga mkono tamko la chama kikuu cha wafanyakazi TUCTA la kupinga makato ya asilimia 15% ya mishahara ya baadhi ya wafanyakazi wanaodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu.

Tunawaomba na kuwasihi madaktari kote Nchini kuendelea kufanya kazi kwa mujibu ya maadili na miiko ya kidaktari ili kutoa huduma bora kwa wagojwa.

IMETOLEWA NA CHAMA CHA MADAKTARI TANZANIA – MAT
 
Siasa taka zinatuvuruga hawa nao wajiangalie wanaweza kuambiwa wanataka kushiriki kwenye siasa kama wale wanasheria..
 
Kufanya kazi kwa mihemuko pasipo kuufuata utaratibu wa kazi,haya yataleta majanga kwa taifa letu,wateule wa rais lazima waelewe mipaka yao ya kazi la sivyo wapewe seminar,hatuitaji sifa za kijinga wengine hata vyeti vya form four hawana,wakati madaktari wetu wame toil kweli kweli to become doctors
 
1742 ma daktari awana ajira ukweli ni kwamba Daktari awezi kukosa ajira hata serikali ukisema iwaajiri kati ya 1742 itawapata chini ya 300
 
Kufanya kazi kwa mihemuko pasipo kuufuata utaratibu wa kazi,haya yataleta majanga kwa taifa letu,wateule wa rais lazima waelewe mipaka yao ya kazi la sivyo wapewe seminar,hatuitaji sifa za kijinga wengine hata vyeti vya form four hawana,wakati madaktari wetu wame toil kweli kweli to become doctors
Ni kwa sababu taifa hili tumekubali kuganywa kwa sababu za kushabikia vyama badala ya kuishabikia Tanzania, ukweli ni kwamba awamu hii imelivuruga vibaya taifa hili. Na kama hali hii haitadhibitiwa na sisi wananchi wenyewe, wakati awamu hii inamaliza muda wake taifa tayari litakuwa vipande vipande. Hawa ma-dc na ma-rc wamegeuka kuwa miungu watu, na huku nje ya kamera wanadai wanatekeleza maelekezo ya mkuu! Sasa kama ni kweli hicho ndicho mkuu anawaelekeza wafanye basi twafaa!
 
Kama Docs wapo serious wangemualika Bwana mkubwa kwenye function ya madaktari na kutoa dukuduku lao lakini hizi press release huwa hazichukuli positive nasema haya kama Docs wanataka kusikilizwa lakini kama wanataka siasa basi waendelee na style hii.
 
Mbona tukio la kunyanyaswa dr. Kimwelu wa hapa dar mpaka akajiuzuru hujalitaja
 
KUWEKWA NDANI KWA UZEMBE KAZINI NI JAMBO LA KUPONGEZWA, LAKINI KUWEKWA NDANI KWA UONEVU NI JAMBO LISILOVUMILIKA HATA KIDOGO.
 
Mkuu hapo kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha umepotosha.....mganga mkuu ana wajibu wa kujua ni mtumishi yupi anadai nini na ni nini kikwazo cha mtumishi husika kutokulipwa stahili husika kwa kushirikiana na katibu wa afya wilaya kumpa mkurugenzi madai hayo....sasa kilichotokea Monduli ni wauguzi kumlalamikia Gambo kuwa kila wanapodai madai yao mganga mkuu wa wilaya amekua anawaambia wajaze fomu ndipo Gambo kumuuliza kulikoni??.....ina maana haya madeni ya hata watu hamna ama ni kuwasumbua tu??.....na akashauri wawe na database ya madeni na pia mganga mkuu awe na tabia ya kumkumbusha mkurugenzi pindi wapatapo hela walipe madeni ya watumishi.
 
Pamoja na taaluma zenu, msisahau kuwa ninyi ni watu kama watu wengine, tatizo kuna wenzenu kama walivyo watu wengine, hawana utu wala hawajali thamani ya utu wa mtu mwingine, mjitathmini pia maana moja ya kundi linalojiona Miungu watu ni pamoja na kundi hili la madaktari wachache wanaodharau watu!
Mimi yaliwahi kunitokea na kwa kweli nililia sana kuona kuna madaktari wakatili wasiokuwa na huruma!
Chama chenu kiwe kinashughulikia pia matatizo yatokanayo na wanachama wao pia, ujumbe kwa watendaji wa serikali umewafikia kupitia tamko lenu, ahsanteni!
 
Tatizo raisi alishasema watumishi wa umma ndio mlilifikisha hapa taifa hili.Hivyo wa kulaumiwa ni jpm kwani yeye mwenyewe ndie kinara wa kunyanyasa watumishi na kubariki unyanyasaji unaofanywa na makonda na wakuu wengine wa mkoa na wilaya kadhalika yeye ndie hakuwapa semina elekezi wateule wake ambao wengi wanadhani matamko na ubabe ndio uongozi bora.Yaani nchi hii aina zote za ufisadi zimefanywa na wanasiasa na hata mikataba yote mibovu imeshinikizwa kufanyika na wanasiasa na hata bajeti na miswada isiyo na maslahi kwa taifa imefanywa na wanasiasa,manunuzi yasiyo na tija ya vitendea kazi na miundombinu ya serikali hufanywa na kushinikizwa na wanasiasa,pia idara ya elimu yaani mfumo mzima wa elimu unaosababisha kutoa bota elimu kwa shule za serikali ni matokeo ya mipango ya wanasiasa ya sera na bajeti, Sasa anapotokea kiongozi na kuamini kuwa wanasiasa hawana matatizo bali tatizo kuu lililokwamisha maendeleo ya nchi hii ni watumishi wa umma tu hivyo wao ndio wanapaswa kuhakikiwa na kufanyiwa vitisho na unyanyasaji na kufukuzwa kazi kama vibarua wasio na mikataba ni hatari sana na ni uonevu wa kiwango cha juu kabisa kwa kundi unalojua hawana la kukufanya.Mbona jwtz,polisi, wanasiasa ,na viongozi wa umma hawadhihakiwi wala kuhakikiwa?
 
Back
Top Bottom