Taarifa kwa umma: Usambazaji wa taarifa za kughushi

Taarifa kwa umma: Usambazaji wa taarifa za kughushi

Joined
Mar 27, 2025
Posts
33
Reaction score
45
TAARIFA KWA UMMA

Dodoma; April 25, 2025

Kumekuwa na wimbi la taarifa mbalimbali kwa umma zinazozambazwa kwenye mitandao ya kijamii ambazo zinaonyesha kutolewa na Baraza la Famasi. Baraza linapenda kuutarifu umma kuwa taarifa hizo ni za kughushi na hazijatolewa na Ofisi ya Msajili.

Tunapenda kuufahamisha Umma kuwa taarifa rasmi za umma zinatolewa kupitia mitandao ya kijamii ya Baraza ambayo inajumuisha Instagram (pharmacy_council_tanzania), Twitter (Pharm_Council), Facebook (Pharmacy Council – Tanzania) na tovuti ya Baraza (www.pc.go.tz). Ni vema umakajiridhisha uhalali wa taarifa mbalimbali za kwenye mitandao kupitia akaunti tajwa hapo juu.

Aidha, ufuatiliaji unaendelea ili kubaini chanzo cha taarifa hizo na pindi itakapobainika, hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote anayehusika.

61f0dced-00df-4571-986d-b06d2ad9a2d2.jpeg


Pia soma Baraza la Famasi linapenda kuutarifu Umma kuwa taarifa ya ziara kwa Vyuo vya Famasi Dar es Salaam ni ya UONGO hivyo ipuuzwe
 
Hao wazushi ni kuwakamata tu... Wengi ni matapeli.
 
Back
Top Bottom