Taarifa kwa Umma Kuhusu Hali ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)

Malcolm X5

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
1,637
2,747
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MFUKO WA TAIFA WA HIFADHI YA

JAMII (NSSF)

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusu hali na mwenendo wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Taarifa hizo zimesababisha hofu na taharuki miongoni mwa wanachama wa NSSF na wadau wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, kwa kuhofia usalama wa mafao yao.

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) inapenda kuwaondoa hofu wanachama wote wa Mfuko wa NSSF na Wananchi kwa ujumla na kuwahakikishia kwamba Mfuko wa NSSF unaendelea kulipa mafao ya wanachama kama kawaida. Kama mnavyofahamu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekwishamteua Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Prof. Godius Kahyarara na anaendelea na majukumu ya kuendesha shughuli zote za Mfuko.

SSRA kwa mamlaka iliyopewa chini ya Kifungu cha 6(2) (c) cha Sheria Na.8 ya mwaka 2008 kikisomwa pamoja na vifungu vya 40 na 48 vya Sheria hiyo, inafanya kaguzi za Mifuko yote ukiwemo Mfuko wa NSSF kwa lengo la kuhakikisha kwamba Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inaendeshwa kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni ili kulinda maslahi ya wanachama na Taifa kwa ujumla.

Kwa mara nyingine, Mamlaka inapenda kuwahakikishia wanachama wote wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii na wadau wote wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kuwa Mamlaka inaendelea kuchukua hatua stahiki kuhahakikisha kwamba michango ya wanachama ipo salama, maslahi ya wanachama yanalindwa na Sekta inabaki imara.

Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii S.L.P 31846

Tovuti: www.ssra.go.tz Dar es Salaam
 
Mbona hakuna taarifa kuhusu malalamiko ya fao la kujitoa ambalo ndilo limelalamikiwa sana na wanachama
 
nyie ssra mmeshindwa kazi aisee, kwa nini kule kwingine wamefuta fao la kujitoa? mko wapi hii mifuko inafanya miradi mingi isiyonufaisha wanachama moja kwa moja?
 
Hii habari ni ya muda mrefu na sioni uhusiano wake na hoja nzito ya fao la kujitoa. Mleta mada tueleze kidogo ulitaka kuutuaminisha kitu gani?
 
Back
Top Bottom