TAARIFA KWA UMMA: CHADEMA Watoa msimamo kura ya maoni ya Katiba mpya

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wanaJF,
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Leo 28.04.2016 wametoa taarifa rasmi yenye msimamo juu ya kura ya maoni ya katiba mpya. Aidha nimeambatanisha nakala katika mfumo wa PDF.

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vincent Mashinji amesema kuwa Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi ndiyo msingi imara pekee unaoweza kuweka mifumo na taasisi kwa ajili ya maendeleo ya kweli yatakayogusa maslahi ya Watanzania wote badala ya nchi kuongozwa na kauli za viongozi.

Kutokana na umuhimu huo wa kuzingatia maoni ya wananchi yanayobeba matakwa yao katika mchakato wa Katiba Mpya, amesema kuwa CHADEMA hakitashiriki Kura ya Maoni ya Katiba Mpya Inayopendekezwa ambayo ilipitishwa na Bunge Maalum la Katiba baada ya kubadili na kuondoa mapendekezo yaliyotolewa na wananchi kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya.

Badala yake, CHADEMA kitaendelea kuweka agenda ya kupigania Katiba Mpya na bora katika vipaumbele vyake, kwa sababu itatibu vidonda na kumaliza makovu yaliyoko katika jamii kutokana na matatizo mbalimbali kama vile ukosefu wa haki, migogoro ya ardhi, wananchi kukosa huduma za msingi za kijamii zikiwemo elimu, maji na afya.

Dkt. Mashinji ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipoukaribisha ujumbe wa Chama cha Centre Party cha Norway uliofika ofisini kwake jijini Dar es Salaam kutia saini makubaliano ya ushirikiano kati ya vyama hivyo kwenye Mradi wa Elimu ya Demokrasia awamu ya pili unaofanyika Wilaya ya Mtwara Vijijini.

Dkt. Mashinji pia amekishukuru chama hicho kwa kusaidia kutoa elimu ya uraia kwa Watanzania hususani maeneo ya vijijini katika mradi ambao unahusisha vyama vyote vya siasa vyenye uwakilishi ndani ya Bunge, huku akisisitiza kuwa CHADEMA kiko tayari kwa ushirikiano unaozingatia maslahi na matakwa ya wananchi hasa katika kukuza uelewa wa kudai haki, demokrasia na uongozi bora ndani ya nchi.

“Suala la Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi kama ilivyowasilishwa kwenye rasimu ya pili na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya ni agenda muhimu kwa Watanzania wapenda nchi yao na sisi ni kipaumbele kwa mwaka huu na kuendelea hadi hapo nchi yetu itakapopata Katiba Mpya ya Wananchi.

“Jana na leo tumewasikia baadhi ya viongozi wa serikali wakisema kuwa wanajiandaa kuitisha kura ya maoni…hatutashiriki kura ya maoni ya Katiba Mpya Inayopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba. Tunajua Watanzania wengi wanataka Katiba Mpya iliyotokana na maoni yao, si ile iliyochakachuliwa bungeni.

“Katiba Mpya iliweka masuala kuhusu haki za wananchi, kuimarisha misingi na kuweka mifumo ya demokrasia na uongozi bora, walau kwa kuanzia. Hatuwezi kusema sasa tutatumia mikakati gani kuwahamasisha Watanzania kuidai Katiba Mpya…tutajua namna ya kuvuka tukishafika mtoni,” amesema Katibu Mkuu Dkt. Mashinji.

Aidha, Katibu Mkuu Dkt. Mashinji amesisitiza kuwa suala la nchi kuwa na misingi na mifumo imara ya demokrasia na uongozi bora ni muhimu kwa Tanzania, katika wakati ambapo nchi inaelekea kwenye uchumi mkubwa wa nishati ya gesi na mafuta, akisema vinginevyo ni hatari iwapo taifa lenye utajiri mkubwa wa rasilimali, litaendelea kuwa na wananchi waliokata tamaa kutokana na mfumo mbovu uliopo.

Akisisitiza umuhimu wananchi kuwa Katiba inayotokana na wananchi, Dkt. Mashinji alitolea mfano wa nchi ya Norway ambayo miaka mingi nyuma ilikuwa sawa na Tanzania, lakini ilifanikiwa kuondokana kuwa taifa maskini kutokana na uwepo wa uongozi bora, mifumo na taasisi imara za kidemokrasia ambazo ziliweza kusimamia ustawi wa taifa hilo kutokana na uchumi wa gesi na mafuta na sasa ni kati ya mataifa yaliyoendelea barani Ulaya na duniani kwa ujumla.

Kwa upande wake ujumbe huo uliokuwa ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Centre Party, Knut Olsen, umesema kuwa chama hicho kinashukuru kwa mradi huo kuingia katika hatua ya pili kuanzia mwaka 2016-2019 huku hatua ya kwanza ikiwa na mafanikio makubwa katika jamii ya wananchi wa maeneo ya pembezoni.

“Kama unavyojua, mradi huu kupitia TCD unahusisha vyama vyote vyenye uwakilishi ndani ya bunge, na lengo letu ni kuwajengea uwezo viongozi wa vyama hasa wanawake na vijana katika ngazi ya jamii kwenye vitongoji, vijiji, kata na bunge ili waweze kushiriki mchakato wa maamuzi. Tunatarajia kuendelea kupata ushirikiano katika hatua ya pili,” amesema Inger Bigum, ambaye ni Meneja wa Mradi hapa nchini.

Wengine waliokuwa katika ujumbe huo wa Centre Party ni pamoja ni Katibu Mkuu wa Vijana Sara Hamre, Katibu Mkuu wa Wanawake, Eline Stokstad-Oslan na Katibu Mkuu wa Wazee, Kristin Madsen.

Mradi huo wa Elimu ya Demokrasia katika Wilaya ya Mtwara Vijijini unaohusisha vyama vyenye uwakilishi bungeni kupitia Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) chini ya ufadhili wa chama hicho, katika awamu ya kwanza ulihusisha kata za Msangamkuu, Nanyamba, Ziwani na Mbembaleo na katika sasa awamu ya pili utakuwa katika kata za Mkunwa, Tangazo, Mayanga na Madimbwa.

Imetolewa leo Alhamis, Aprili 28, 2016 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
 
Attachments

  • MSIMAMO KURA YA MAONI KATIBA MPYA.pdf
    35.7 KB · Views: 117

Hapa ndio tunaposhindwa ona mbali, kususia ndio CCM wanachotaka iliwapitishe, nilishasema katiba hii ingelipita kabla ya uchaguzi Chadema wangelikuwa madarakani kwani kuna mambo Fulani tungelipata harafu tungeibadili kwa matakwa ya tume. Mambo yahoo ni tume huru na matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani. ilikuteka inchi lazima uanze na kalia angalau mita moja ya mlaba, na nyingine na nyingine.
 
Hii ni kura ya maoni ya wananchi,chadema hawana sababu ya kuhofia maoni ya watanzania.

Ni kura ya maoni tu ,na maoni ya wananchi ni ya kuheshimiwa kuliko hivyo vyama vya siasa
 
na dhani ni vyema kuanza kutoa elimu kwa wananchi na elimu hiyo kama mnataka wananchi wafanye maamuzi sahihi msiingize itikadi ndani.

yaani ukisimama kwenye jukwaa unasema katiba ni ya chama fulani na chama fulani ndio wanaleta haya unashawishi upande mwingine na wao kuchukua upande tofauti na kuanza kukupinga maana hapa kinachokuwa kikipingana sio katiba tena bali ni itikadi za vyama.

kama tunataka mageuzi ya kweli ya katiba tuache propaganda katika mchakato na pengine katiba mpya ikisha patika ndio kila mmoja anaweza kujigamba kwa amchango aliouweka.

kuingiza itikadi katika hili ni jambo lilo wazi kuwa tutakuwa tunatafuta njia za dhati kuukwamisha maana tunashikamanisha mchakato wa katiba na ustawi wetu wa kisiasa. tunawapa changamoto wanaofanya maamuzi ama wachague kufanya maamuzi sahihi na kutubeba sisi kisiasa au wachague kufanya tofauti.

ni kubadili msimamo na kuingia katika mchakato kwa kutoa elimu stahiki kwa wananchi.

je wananchi wakiikataa katiba inayopendekezwa mtaibuka na kujiunga au
 
Denominator ya kukotoa itakuwa ni watu wote waliopiga kura na numerator wale watakaoikubali hivyo hao ambao hawatoshiriki hawatoathiri chochote kupitishwa kwa katiba. Walifanya kosa kubwa kususia bunge la katiba. Pengine maoni yao yangefanya ipatikane katiba bora.
 
kwani chadema c wananchi
Mwananchi si kuishi tu ndani ya nchi. CHADEMA kibaraka wa wazungu.Ona Katibu mkuu alivyobwabwaja alipokutana na hao wanorway!! Siku zote alikuwa haongei kuona tu mzungu kaongea hadi basi

Chama hakina uwezo wa kumshinikiza mpiga kura asiende.
Wakisusa poa tu inaonyesha somo la CUF kususa Zanzibar halijawaingia hawa CHADEMA.

Katiba ya nchi sio ya CHAMA
 
Kwa nchi hii haiwezekani wananchi hata wakipinga hiyo katiba iliyochakachuliwa bungeni serikali watafosi tu sababu ni wezi hawawezi kuikubali katiba ya walioba sababu inawabana wezi na ukizingatia serikali yetu wengi ni vibaka kwa hiyo watafanya kila namna waipitishe katiba yao na waendelee kutuiba.
 
Hivi tabia za kike za kuzila mtaziacha lini? Kwa nini msihamasishe wananchi kuipigia kura ya hapana? Mkizira ndo inapita na tunakuwa tumeliwa wote. Msingezila bunge la katiba hata huu upupu wa katiba inayopendekezwa usingekuwepo.
 
Kwani kura ya maoni inapigiwa kura na vyama? Kwani CHADEMA ina kadi ya kupigia kura?

Wanaopiga kura ni wananchi.wananchi Tutapiga hakuna tatizo.
Hauwezi kuwatenganisha wana Nchi (wa Tanzania ) na CHADEMA
 
Hivi kwa nini Masoud Kipanya hachori kikatuni cha chadema kikizama matopeni, kila tawi kikishika linakatika sasa limebaki tawi moja la katiba kikatuni kimelishikilia desperately??
 
Hii ni kura ya maoni ya wananchi,chadema hawana sababu ya kuhofia maoni ya watanzania.

Ni kura ya maoni tu ,na maoni ya wananchi ni ya kuheshimiwa kuliko hivyo vyama vya siasa
Wananchi = CHADEMA FYI
 
Kwa nchi hii haiwezekani wananchi hata wakipinga hiyo katiba iliyochakachuliwa bungeni serikali watafosi tu sababu ni wezi hawawezi kuikubali katiba ya walioba sababu inawabana wezi na ukizingatia serikali yetu wengi ni vibaka kwa hiyo watafanya kila namna waipitishe katiba yao na waendelee kutuiba.
katiba inayopendekezwa ilipigiwa kura ndani ya bunge la katiba,hatua iliyobaki ni wananchi kupiga kura ya maoni,
kama wataikataa tunarudi kutumia katiba ya sasa.
Kama kutakuwepo na uwezekano wa kuanza utaratibu mpya mpaka ipatikane katiba wanayotaka UKAWA then hilo ni suala la kuvuta subira pengine baada miaka 30 au 40
 
Mahaba niuwe a.k.a wafia chama/Lumumba7000.com
 
Back
Top Bottom