Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Taarifa ya Ziada kutoka Waziri Kivuli wa Mambo ya nje Mch. Peter Msigwa kuhusu Ufadhili wa MCC
UKWELI KUHUSU MCC NA MISAADA KWA TANZANIA
Baada ya Tanzania kunyimwa msaada wa Shilingi Trilioni Moja na Shirika la Kimarekani la Millenium Challenge Corporation (MCC), viongozi wa kiserikali, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Agustine Mahiga, Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na makada kadhaa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kama Humphrey Polepole, kila mmoja kwa wakati wake, wamejaribu kuwapotosha na kuwapumbaza Watanzania, wakijaribu kupenyeza propaganda na uongo wa aina kuu tatu:
• Kwanza, Wanajifanya wao ni Wazalendo kwelikweli na kudai kuwa “Uhuru wa Tanzania hauwezi kuingiliwa wala kuthaminishwa kwa Shilingi Trilioni Moja za Kimarekani”. Na kwamba watahakikisha maendeleo ya Tanzania yanashughulikiwa kwa kuongeza “mapambano dhidi ya rushwa na kukusanya kodi kwa wingi”.
• Pili, wanadai Serikali ya Tanzania haitaki misaada na haitaathirika kwa namna yoyote ile kwa kunyimwa msaada huo. Waziri wa Fedha, Dk Philip Mpango alifikia hatua ya kusema kuwa “hata bajeti ijayo ya serikali haikuzijumuisha fedha hizo za MCC”, na kwamba bajeti ijayo itajitosheleza bila kutegemea fedha za MCC.
• Tatu, wanajikanganya kwa kudai kuwa uamuzi wa MCC haukuwa wa haki – Tanzania ilionewa. Hapa, Waziri Mahiga alidai kuwa MCC walipaswa kujadiliana kwanza na Serikali kabla ya kusitisha msaada huo. Mahiga alikwenda mbali zaidi akidai “demokrasia ya Tanzania haiwezi kupimwa kwa kutazama uchaguzi wa Zanzibar tu” na kusisitiza kuwa Tanzania ni nchi inayofuata utawala bora na demokrasia.
Kwa nafasi yangu kama Waziri wa Mambo ya Nje wa Upinzani, Mbunge na Mzalendo wa Kweli wa Taifa hili, nachukua fursa hii kwa mara nyingine tena kuwaeleza Watanzania ukweli dhidi ya uongo na upotoshwaji mkubwa uliofanywa na Wana-CCM hao bila kujali maslahi ya Watanzania na Mustakabali wa Taifa hili:
Ukweli Unaopotoshwa:
1. Nianze na suala la uzalendo. Wanaojifanya Wazalendo kwa kupinga uamuzi wa MCC, si wazalendo wa kweli wa nchi hii – ni Wazalendo Uchwara.
Uamuzi wa MCC kusitisha msaada kwasababu ya kuchukizwa na uchaguzi haramu wa marudio kule Zanzibar na Sheria kandamizi ya makosa ya mitandaoni (Cyber Crime) iliyoipitishwa kibabe na Serikali hii, ulikuwa ni uamuzi sahihi na uliojali maslahi endelevu si tu ya watu wa Taifa hili bali ya maslahi ya Dunia hii. Chaguzi haramu kama ule wa Zanzibar zinaweza kabisa kuchochea matukio ya ugaidi, vita vya wenyewe kwa wenyewe na kukwamisha maendeleo kwasababu ya kulazimisha kuweka viongozi madarakani kimabavu bila kujali hatima endelevu ya Taifa na Dunia kwa ujumla. Demokrasia na Uhuru wa Watu ndiyo rutuba kuu ya kupata maendeleo makubwa, ya maana na endelevu.
“Ni uwendawazimu kwa Mtanzania yeyote yule kujifanya anatetea “uzalendo” wa Taifa lake kwa kushambulia Mataifa na Mashirika ya nje, kwa suala ambalo Serikali yetu yenyewe ndio inayokandamiza demokrasia na kuminya uhuru wa watu wa Taifa hili”
“Uzalendo si kupinga kila kitu kinachotendwa au kuamuliwa na watu au taasisi za Taifa jingine, bali ni kupinga udhalimu wa aina yoyote ile bila kujali unatendwa na nani; uzalendo wa kweli si kupinga mataifa na mashirika ya kigeni bila sababu za msingi, bali ni kupinga udhalimu unaofanywa na yeyote yule, ukiwemo udhalimu unaofanywa na Serikali yetu dhidi ya watu wa Taifa hili; uzalendo ni kusimamia mambo ya msingi na kupinga mambo ya hovyo”.
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema:
“Kaburu ni Kaburu tu….hata awe na rangi nyeusi…bado anabaki kuwa ni Kaburu tu”
Hatuwezi kutetea udhalimu wa Serikali yetu eti kwasababu tu watu wa nje wamechukua hatua dhidi ya serikali yetu. Serikali yetu sio Mungu, ikikosea ni lazima tuikosoe. Tuache kutetea ujinga.
Inasikitisha kuona kuwa Wamarekani na MCC yao wameonyesha uzalendo wa kusimamia mambo ya msingi, kuliko hawa Wazalendo Uchwara wa CCM wanaotetea udhalimu wa serikali hii, bila kujali hasara kubwa ya mahusiano ya kidiplomasia na kimaendeleo wanayoisababishia Tanzania”
Ni ujinga kufikiri kuwa eti Taifa litapata maendeleo ya uhakika kwa mtindo wa kutumbua majipu tu. Matatizo ya Tanzania kamwe hayawezi kufananishwa na mtu mwenye majipu ambapo yakitumbuliwa tu basi matatizo hayo yanakwisha – hapana. Kama ni ugonjwa, basi Tanzania yetu inaugua Kansa na Kansa haitumbuliwi. Kansa hushughulikiwa kwa kupiga mionzi au kukata viungo.
Kansa inayoitafuna Tanzania ni Kansa ya kuwa na mfumo kandamizi wa kiutawala na kisheria; mfumo unaowaminya watu uhuru wa kujiwekea serikali na viongozi bora wanaowataka; mfumo unaowanyima Watanzania uhuru wa kuikosoa na kuiwajibisha vizuri serikali yao; ni mfumo huu mbovu unaoipa CCM jeuri ya kufanya itakavyo ndio uliosababisha MCC kusitisha misaada. Wenzetu wanajua fika hakutakuwa na tija kutoa msaada kwa serikali yenye vijinasaba vya udikteta kama hii – udikteta na maendeleo havipatani - ni Mbingu na Ardhi!
2. Nizungumzie na kauli za hovyo.
Eti “serikali haitaki misaada” kama alivyosema Waziri wa Fedha Dk. Philip Mpango na kudai kuwa “Tanzania haitaathirika kwa kukosa fedha za MCC”
Ukweli ni kwamba kuna tofauti kubwa sana kati ya kukataa msaada na kunyimwa msaada. Kukataa msaada ni heshima lakini kuomba msaada na kunyimwa ni aibu kubwa. Tanzania iliingia kwenye program ya kusaidiwa na MCC. Haiwezekani Serikali inyimwe fedha kwa kushindwa kutimiza vigezo halafu viongozi wa kiserikali na CCM wajifanye hawakuzitegemea fedha hizo.
Tanzania si tu ilizitegemea fedha za MCC, bali pia bado inategemea misaada ya nchi na mashirika mbalimbali ya kimataifa.
Kwa mfano, wakati mawaziri wakidai kuwa wanaanza kuiendesha nchi hii hivi sasa bila kutegemea misaada, hali halisi ya sekta ya afya inaonyesha kuwa kwa muda mrefu mashirika mbalimbali ya kimarekani ndiyo yamekuwa yakinusuru afya za Watanzania kuliko serikali yetu.
Hapa nchini kuna NGOs nyingi za kimarekani zinazotekeleza miradi ya afya zaidi ya 50 kwenye maeneo mbalimbali. Mashirika hayo ni kama Johns Hopkins, FHI 360, White Ribbon Alliance na maengineyo. Baadhi ya miradi wanayoitekeleza inahusu kusaidia ununuzi na ugavi wa dawa nchini; kuwajengea uwezo watoa huduma za afya nchini, hasa kwenye eneo la afya ya mama na motto, kuelimisha jamii jinsi ya kubadili tabia na mienendo ili kujikinga na magonjwa ya zinaa na milipuko kama Ukimwi na kipindupindu na mengineyo, na miradi mingine inahusu kuboresha zahanati na vituo vyetu vya afya kwenye maeneo mbalimbali nchini. Hii ndiyo kusema kuwa ni ujinga wa hali ya juu kuwa na viongozi wa serikali wanaoongea uongo usiokuwa na faida yoyote ile kwa Watanzania. Ikitokea nchi zote wahisani, mashirika ya misaada na NGO’s zao za kimataifa zikaacha kuisaidia Tanzania ni dhahiri kuwa hali itakuwa ni mbaya sana kwa Wananchi walio wengi.
Mathalan, takwimu zinaonyesha kuwa nchini Tanzania mwanamke mmoja kila saa anapoteza maisha kwasababu ya kukosa huduma bora za afya wakati akiwa mjamzito na wakati wa kujifungua. Kwa maneno mengine, takribani wanawake 24 nchini Tanzania hupoteza maisha kila siku na takribani wanawake 9,000 hupoteza maisha kila mwaka si kwasababu Mungu amependa, bali kwasababu serikali ya CCM kwa muda mrefu imeshindwa kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto nchini.
Aidha, takwimu za utafiti wa Hali ya Idadi ya Watu na Afya – Demographic and Health Survey” wa miaka ya hivi karibuni, zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 42 ya watoto wote nchini wamedumaa, hasa kwasababu ya utapiamlo au lishe duni. Idadi hii ni kubwa mno na inatishia mustakabali wa Taifa. Mtoto aliyedumaa akili yake haitaweza kufanya kazi kwa ufanisi kwa asilimia mia moja. Hii inasababisha Tanzania kuwa katika hatari ya kuwa Raslimali Watu wasioweza kuzalisha kikamilifu na hivyo kuathiri zaidi ukuaji wa uchumi na maendeleo ya jamii.
Mashirika mengi ya kimataifa, yakiwemo ya Marekani, Uingereza, Ujerumani, Uholanzi, Canada ndiyo yanayojaribu kuisaidia Tanzania kuboresha huduma za afya na kupunguza vifo vingi vinavyoepukika na kutekeleza miradi ya kuimarisha huduma za lishe ili kupunguza udumavu wa watoto kwenye yetu. Kwa mantiki hii, ni ujinga wa hali ya juu kwa viongozi wa serikali hii kujifanya hawataki misaada, wakati wanajua ukweli kuwa bado nchi yetu inahitaji misaada wakati ikijaribu kujikongoja ndipo tuweze kujitegemea
Nasisitiza kuwa Tanzania si kisiwa na kamwe haiwezi kuishi kama kisiwa - tunahitaji kushirikiana vema na mataifa mengine, kufanya kazi kwa karibu na mashirika ya ndani na ya kimataifa katika kusukuma maendeleo yetu na maendeleo ya dunia. Hii ni dunia ya kutegemeana na kuhitajiana, si kifedha tu bali kuingiliana vizuri kibiashara, kimisaada na kidiplomasia. Serikali yetu imekosea, inapaswa kujirekebisha, iache kiburi. Kiburi si maungwana
Hatua ya Mawaziri wa Magufuli kudai kuwa Tanzania haitaathirika kwa kuzikosa Trilioni Moja za MCC ni ujinga mwingine uliopitiliza. Ni lazima tutaathirika kama ifuatavyo
• Fedha za MCC zilikuwa zielekezwe kwenye miradi ya umeme vijijini kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA). REA ina wafanyakazi zaidi ya 450, kusitishwa kwa msaada huo kunaweza kuharibu ajira za Watanzania wenzetu na familia zao.
• Uchambuzi wa taarifa za serikali yenyewe unaonyesha kuwa gharama ya mtu kufungiwa umeme ilianza kupungua hadi kufikia shilingi 67,000. Hatua ya MCC kusitisha msaada wake inaweza kusababisha gharama za kuwafungia watu umeme vijijini kupanda sana na Watanzania wengi wanaweza kuendelea kubaki gizani kwasababu ya kushindwa kumudu gharama hizo.
• Ipo hatari kwa serikali hii kupandisha viwango vya kutoza kodi kwenye bidhaa na huduma mbalimbali ili kujaribu kupata fedha za kufidia pengo la fedha zilizokuwa zitolewe na MCC. Hali hiyo itatuweka Watanzania kwenye mzigo mkubwa wa gharama za kulipa kodi na kusababisha makali ya maisha kwasababu tu ya uchu na ulevi wa madaraka wa serikali ya CCM.
• Ni vema Watanzania wakaacha kurubuniwa na CCM iliyoshindwa kutatua matatizo yao kwa muda mrefu. Trilioni moja ni fedha nyingi sana. Ni 5% ya bajeti ya nchi yetu..
Ukichukua Trilioni 1 ukaiweka kwenye noti za elfu 10 utapata jumla ya noti 100,000,000. Kila noti ina urefu wa sentimita 12. Kwa hiyo tukizidisha tunapata sentimita 1,200,000,000 (100,000,000×12). Kilomita 1 ni sawa na sentimita 100,000. Kwa hiyo tukichukua sentimita 1,200,000,000 tukagawanya kwa 100,000 tunapata kilomita 12,000. Umbali wa kutoka Johanesburg (Afrika kusini) hadi Cairo (Misri) ni kimomita 6,259. Kwa hiyo kilomita 12,000 ni sawa na kutoka Johanesburg hadi Cairo mara mbili.
Maana yake ni kwamba ukiweka Trilioni 1 katika noti za elfu 10 unaweza kuzipanga kuanzia Johanesburg hadi Cairo mara mbili bila kuacha hata sentimita moja njiani.
Yani uchukue noti za elfu "kumi" uzipange kuanzia Johanesburg upande nazo hadi Botwsana, kisha Harare, Lusaka, Tunduma, Dar, Nairobi, Khartoom, hadi Cairo bila kuacha hata sentimita moja njiani, kisha ukifika Cairo unaanza tena upya kuzipanga kwa kurudi hadi Johanersburg. Hizo ndio fedha ambazo Marekani wametunyang'anya baada ya kufanya uhuni kule Zanzibar na kupitisha sheria kandamizi bila kujali.
Ni wakati wa kuacha kushabikia utumbuaji majipu wakati Taifa linaugua Kansa - Kansa haitumbuliwi!. Tanzania yetu itapona kwa kufanya mageuzi makubwa ya kimfumo na kujenga nidhamu na haiba njema katika diplomasia ya kimataifa. Hii ni dunia ya kutegemeana na kuhitajiana, si kifedha tu bali kuingiliana vizuri kibiashara, kimisaada na kidiplomasia.
Hata mataifa tajiri kabisa duniani hayakufika hapo yalipo kwa jitihada zao yenyewe, yalitegemea pia mataifa na mashirika ya kimataifa. Tunapaswa kujenga uwezo wa kujitegemea huku tukitegemeana na wenzetu. Tunataka kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama India na Malaysia...hata .hawa tunaotaka kuwafikia nao walisaidiwa na bado wanasaidiwa. India ni moja ya nchi zilizo kwenye programu ya kusaidiwa na MCC
3. Napinga pia madai mengine ya uongo kuwa Tanzania tulionewa. Hatukuonewa. Serikali yetu ilivijua vizuri na mapema vigezo vyote vya kupata fedha za MCC, lakini ilipuuza kwa sababu ya kuendekeza uchu na ulevi wa madaraka.
Mwisho.