Taarifa: Kundi la wakabaji waenda Vikindu kumzika mwenzao

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
4,873
1,216
Jamani naomba niwape taarifa hii,itawasaidia na polisi kwenye kazi zao za kila.katika kupambana na uhalifu hili litamsadia mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.

Ni kwamba kijana ajulikanae kwa jina la Shabani Tampa alimaarufu boxer yaani boxer pikipiki kwa umahiri wake wa kukimbia, jana ameuawa maeneo ya Mwananyamala alipoenda kupora akiwa na mwenzake ambaye hakufahamika jina kwa haraka zaidi.

Kijana ni mkabaji na mwizi aliebobea kutoka Keko Magurumbasi, na nyumbani kwao ni mtaa mrefu karibu na bar iitwayo saja, saja ni maarufu kwa biashara ya ukahaba inayofanyika hapo na kituo kikubwa cha wakabaji wa Keko Magurumbasi.

Taarifa yangu hasa ni kuwajulisha wakazi wa Vikindu kuwa kijana Boxer amekuja kuzikwa Vikindu na amekuja kuzikwa kwa asilimia 80 ni wakabaji wenzake kutoka camp ya home boys Keko mwanga, ambayo ndio maskani kubwa wakabaji wakorofi na wababe.

Wakazi Vikindu muwe makini.

Polisi kama mnahitaji taarifa hizi, anzeni na magari hayo ambayo yamewabeba vijana wengi sana, mtoa taarifa wangu hakunipa namba za magari, ila ni mabasi ya eicher mawili. Basi lilipakia wanaume tupu hao wote ni wezi kwa asilimia 80.

......Yangu ndiyo hayo.

Salamu zangu kwa mkuu wa mkoa, Keko imeshindikana, tatizo kubwa uhalifu huu ni baadhi ya polisi kutoa siri za watoa siri kwa polisi, ndio maana watu wamekua waoga.

Kama imeshindikana kabisa basi waruhusiwe wanajeshi wengi kuishi maeneo yenye vibaka wengi.
 
Keko ni hatari polisi wanajua hili ila hawajaamua kuwakamata -ujumbe umefika
 
Unajua hapa ndio huwa naganda kwenye kazi za kipolisi.
Yaani Keko si leo ni miaka telee,tena Vibaka na wakabaji wa kule sio kwamba wanajificha,wanajulikana mpaka makwao.
Ukienda kutoa taarifa polisi,yaani ni sekunde tu wanakuja kukuambia kwamba mkuu umetoa issue,sasa zam yako.Yaani kuna link nzuri sana ya miaka mingi na ya kihistoria baina ya Polisi na Wahuni wa kule,tena unaweza kukuta Kibaka akikamatwa,basi hata kama dhamana ni 1m jamaa ni mahodari kweli kuchanga,watamtoa tu mwenzao.Yaani wapo vizuri kweli kwenye kusaidiana,na akiishatoka mhalifu kwa dhamana,basi kibano chake na mkwala utaenda mwenyewe kufuta kesi.
Keko ni dunia nyingine kabisaa,ukiwa mgeni ukipita tu mitaa fulani unajistukia kabisaa kwamba upo kuzim.
 
Sawa, nimeshawataarifu wenzangu wa kikosi maalumu, tupo njiani tunaelekea Vikindu makaburini...!
 
Jamani naomba niwape taarifa hii,itawasaidia na polisi kwenye kazi zao za kila.katika kupambana na uhalifu hili litamsadia mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.

Ni kwamba kijana ajulikanae kwa jina la Shabani Tampa alimaarufu boxer yaani boxer pikipiki kwa umahiri wake wa kukimbia, jana ameuawa maeneo ya Mwananyamala alipoenda kupora akiwa na mwenzake ambaye hakufahamika jina kwa haraka zaidi.

Kijana ni mkabaji na mwizi aliebobea kutoka Keko Magurumbasi, na nyumbani kwao ni mtaa mrefu karibu na bar iitwayo saja, saja ni maarufu kwa biashara ya ukahaba inayofanyika hapo na kituo kikubwa cha wakabaji wa Keko Magurumbasi.

Taarifa yangu hasa ni kuwajulisha wakazi wa Vikindu kuwa kijana Boxer amekuja kuzikwa Vikindu na amekuja kuzikwa kwa asilimia 80 ni wakabaji wenzake kutoka camp ya home boys Keko mwanga, ambayo ndio maskani kubwa wakabaji wakorofi na wababe.

Wakazi Vikindu muwe makini.

Polisi kama mnahitaji taarifa hizi, anzeni na magari hayo ambayo yamewabeba vijana wengi sana, mtoa taarifa wangu hakunipa namba za magari, ila ni mabasi ya eicher mawili. Basi lilipakia wanaume tupu hao wote ni wezi kwa asilimia 80.

......Yangu ndiyo hayo.

Salamu zangu kwa mkuu wa mkoa, Keko imeshindikana, tatizo kubwa uhalifu huu ni baadhi ya polisi kutoa siri za watoa siri kwa polisi, ndio maana watu wamekua waoga.

Kama imeshindikana kabisa basi waruhusiwe wanajeshi wengi kuishi maeneo yenye vibaka wengi.

Watawakamata kwa ushaidi upi?
 
Keko bana ni shida hiyo hatari ni ya kitambo sana kama ni operation labda ifanyike kwa namna nyingine maana vibaka walishakuwa marafiki na hao wasimamizi wa sheria
 
Wakazi wengi wa keko ni polisi wastaafu na waliopo kazini na miongoni wa vibaka hao ni watoto wa polisi so don't expect any miracles until Jesus Christ is back
 
Kwa nini walimuua huyu kibaka tena hadharani? Si wangemkamata, wakampeleka polisi ili apewe nafasi ya kujieleza? Walichofanya ni kinyume na haki za binadam.......kimsingi Kituo cha haki za binadam kimeshatoa tamko kukataza haya mambo!
 
Mkuu! Ukirudia kusoma comment za juu, utagundua jinsi ambavyo jamaa(marehemu) ni kibaka mzoefu, sugu hadi akabatizwa jina la "boxer"; Mtoa hoja mwingine akasema hilo eneo limeshindikana vile vibaka wenyewe ni watoto wa polisi wastaafu. Sitetei wananchi kujichukulia sheria mkononi ila kuna wakati watu wanachoka kwani sheria zenyewe ni kibogoyo na zinavunjwa na wahusika. Ndio yale yale ya "hamna jinsi, inabidi wawaue tu"
 
Back
Top Bottom