Taarifa: Benjamini Netanyahu afanya mazungumzo na kachero mkuu wa idara ya ujasusi wa Misri

Uzalendo Wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
1,119
2,000
Waziri Mkuu wa Israel leo Mei 30,2021 amefanya mazungumzo nyeti na Kachero Mkuu wa Idara ya Ujasusi ya Misri Abass Kamel aliyeongozana na Makachero Waandamizi wa Idara hiyo.

Mazungumzo hayo yalifanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu yaliyopo Jijini Jerusalem.

Viongozi wamejadiliana masuala mbalimbali ikiwemo njia za kukizuia kikundi cha Wanamgambo wa Hamas kisiweze kujiimarisha kutokana na misaada inayotarajiwa kutolewa kwa wakazi wa Gaza.

Bwana Netanyahu pia alisisitiza umuhimu wa kuachiwa kwa Askari na Raia wa Israel wanaoshikiliwa mateka Ukanda wa Gaza.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom