Taarabu Asilia imekufa? Jibu liko hapa..

mshumbullah

Member
Jan 29, 2015
35
23
Leo nimepita kwenye mtandao DW Swahili nikakutana na makala ya kusisimua sana inayohusu taarabu asilia kutoka visiwani Zanzibar..

Napenda sana muziki wa taarabu asilia.. Sielewi kwanini huku bara mziki huu haujapenya kihivyo, lakini burudani ya vinanda na sauti za akina Gamba, Rukia, Fatma na wengineo ni moto wa kuotea mbali..

Nawaomba Wanajamvi tutumie uwanja huu kukumbushana taarabu zilizobamba nyakati hizo..
===========

MAKALA: Nyota zilizoanguka - Wasanii wakongwe wanavyotupwa..

Baada ya kukitumia kipaji chao cha kisanii kuelimisha, kuburudisha na kuzijenga jamii zao, ikiwemo kuzitangaza na kuzihuisha sanaa, fasihi na tamaduni zao, wasanii kwenye mataifa mengi masikini barani Afrika hujikuta wanamalizikia kwenye dimbwi la ufukara, maradhi na ukiwa, huku kazi zao zikiendelea kutumika kuwafaidisha wengine.

Chanzo: Nyota zilizoanguka: Wasanii wakongwe wanavyotupwa | Mada zote | DW.COM | 19.12.2016
 
Back
Top Bottom