TAA ZA BARABARANI ZIWE NA SENSOR.....

Shytown

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2025
Posts
1,250
Reaction score
2,350
KWA MAENDELEO YA SAYANSI NA TECHNOLOGIA Kuendelea kuwa na taa ZA BARABARANI zinazowasha kuruhusu magari hata kama hakuna gari huku upande mmoja ukiwa na magari lukuki yanasubiri, ni matumizi mabaya kabisa ya muda.

1. Nafikiri tuanze kununua taa zenye Sensor, ambayo inawezesha kuona; kama barabara haina magari haiwashi...inawasha ule upande wenye magari tu....
2. Lakini pia, kwa mazingira ya kwetu round about (kubwa) ina ufanisi wa hali ya juu kuliko hata taa za barabarani.
3. Tofauti na taa basi tufikirie kuwa na flyover kwenye highway na kuachana kabisa na taa...pale tunapoweza.
4. Ujenzi wa barabara za highway uzingatie uwekaji wa vivuko vya watembea kwa miguu (vya juu au chini) na sio kuchora mistari kila pahala...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…