Sweden Yampongeza Magufuli, Yaahidi Kuongeza Ufadhili, Uwekezaji na Biashara

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,685
119,325

7/02/2017 By Pascal Mayalla Sweden Yampongeza Magufuli, na Tanzania na Kuahidi Kuendelea Kuisaidia Kufadhili Miradi ya Maendeleo.

Sweden imeipongeza serikali ya Awamu ya 5 inayoongozwa na rais Dr. John Pombe Magufuli, kwa jinsi inavyotumia vizuri misaada ya nchi wafadhili katika miradi mbalimbali ya maendeleo, na kuahidi kuendelea kuisaidia Tanzania katika miradi mingine mbalimbali ya maendeleo.

Pongezi hizo zimetolewa na Balozi wa Sweden inchini Tanzania, Balozi Katarina Rangnitt baakwada ya kukamilika kwa ziara ya wiki moja, ya ujumbe mzito wa watu 10, kutoka nchini Sweden wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Biashara katika Wizara Mambo ya Nje, wa Sweden, Bi Karin Olofsdotter, na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Sweden, Johannes Oljelund baada ya kutembelea kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha pamoja cha mpakani cha kwenye mpaka wa Tanzania na Zambia, Tunduma (One Stop Border Post -OSBP ) kinachojengwa na Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) kwa ufadhili wa Sweden.

Balozi Katarina Rangnitt amesema Sweden imeridhishwa sana na jinsi serikali ya rais Dr. John Pombe Magufuli, inavyotumia fedha za wafadhili katika kuleta maendeleo endelevu, na kuipongeza Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) inavyosimamia vizuri miradi hiyo ya wafadhili ya uwezeshaji wa biashara kwa lengo la kuboresha maisha ya Watanzania kwa kuimarisha mazingira ya kufanya biashara, na kutokana ma matumizi hayo mazuri ya fedha za wafadhili, Sweden na wafadhili wengine, wanahamasika kuzidi kuisaidia Tanzania.

Akishukuru kwa niaba ya TradeMark Tanzania, Mkurugenzi wa Trademark Tawi la Tanzania, John Ulanga, aliishukuru serikali ya Sweden kwa misaada yake nchini Tanzania, na kuendelea kuiaminia TradeMark East Africa kuisimamia, ambapo ujumbe huo umeshuhudia kuanza kwa ujenzi kituo hicho cha pamoja cha mpakani eneo la Tunduma kinachorarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18, na kitapunguza msongamano wa magari mpakani kwa asilimia 30%.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa, aliishukuru serikali ya Sweeden kwa niaba ya Serikali ya Tanzania. Na kusema ujenzi wa kituo hicho ni ukombozi mkubwa kwa mkoa wa Songwe katika kukuza biashara na kuleta maendeleo, ambapo kutapunguza msongamano katika mpaka wa Tunduma, ambao ndio mpaka ulio bize kuliko mipaka mingine yote, msongamano ukipungua, biashara zitaongezeka na mapato yataongezeka.

Mkurugenzi Mkuu wa TMEA, kutoka makao makuu ya TMEA, jijini Nairobi, David Stanton alibainisha kuwa kukamilika kwa kituo hicho cha pamoja mpaka wa Tunduma, pia kutaisisimua kuongezeka kwa matumizi ya Bandari ya Dar es Salaam na waagizaji wa mizigo kwa wafanya biashara wa Malawi, Zambia, DRC, Rwanda na Burundi kufuatia kupungua kwa msongamano wa mizigo bandarini na kuchukua muda mfupi kuivusha mizigo nje ya nchi.

Bwana Stanton, amesema kukamilika kwa kituo hicho, pia kutapunguza gharama za usafirishaji ambapo contena zenye mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam huchukua zaidi ya mwezi mzima hadi siku 45 kurudishwa bandarini, ambapo kila siku zinalipiwa, hivyo muda wa kukaa njiani ulipunguzwa, pia utapunguza gharama za usafirishwa, kuongeza idadi ya mizigo na kuongeza kiwango cha biashara na mapato.

Mkurugenzi Mkuu wa Biashara katika Wizara Mambo ya Nje, wa Sweden, Bi Karin Olofsdotter, amesema, Sweden imeridhika sana na maendeleo mazuri ya misaada yake kwenye miradi mbalimbali nchini Tanzania na kusema ujenzi wa kituo cha OSBP ya Tunduma, sio tuu kinatarajiwa kukuza biashara ya mpakani biashara bali pia kitakuza familia kufuatia wanawake wengi ndio wafanyabiashara wakuu wa biashara ndogo ndogo za mipakani hivyo matokeo muhimu ya miradi hiyo ni kuongezeka Mapato, kuundwa kwa ajira na vipato endelevu kwa wananchi wa Tanzania.

Ujumbe huo pia ulitembelea mradi wa Financial Sector Deepening Tanzania (FSDT) unaofadhiliwa na Sweden umesaidia National Microfinance Bank (NMB) kuendeleza huduma ya simu za kibenki ambayo imesaidia kueneza huduma za kibenki kuwafikia watu wengi zaidi wakiwemo wafanyabiashara na hasa wanawake katika maeneo ya vijijini kupata huduma za kifedh

Tanzania ni moja ya washirika Sweden muda mrefu katika kusaidia maendeleo, kuadhimisha miaka 50 ya ushirikiano katika 2013. Moja lengo ni kupunguza utegemezi wa Tanzania juu ya misaada. lengo la mkakati ni kufikia matokeo thabiti katika maeneo yafuatayo, ambapo wanawake, watoto, vijana na wajasiriamali ni lengo kuu makundi:
1. Ajira zaidi na maendeleo ya nishati na masoko ya kilimo.
2. Elimu Kuboresha na kuongezeka kwa ujasiriamali.
3. Nguvu uwajibikaji wa kidemokrasia na uwazi, na kuongezeka kwa ufahamu wa haki za binadamu.
TradeMark East Africa
TradeMark East Africa (TMEA) ni shirika lisilo la kiserikali, la maendeleo kwa lengo la kuongezeka ustawi wa kiuchumi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa njia ya biashara. TMEA inafanya kazi kwa karibu na taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), serikali za kitaifa, sekta binafsi na asasi za kiraia.
TMEA inachangia ukuaji wa biashara Afrika Mashariki kwa kufungua fursa za kiuchumi kupitia:
• Kuongezeka kwa fursa za upatikanaji wa masoko;
• Kuboresha mazingira ya biashara; na
• Kuboresha biashara ya ushindani.
Kuongezeka kwa kiwango cha biashara kuchangia ukuaji wa uchumi, na kupunguza umaskini na hatimaye kuongezeka ustawi.

TMEA ina makao yake makuu mjini Nairobi nchini Kenya, na ina matawi katika miji ya Arusha, Bujumbura, Dar es Salaam, Juba, Kampala na Kigali.
Paskali
cleardot.gif
 
Asante Mkuu Paskali kwa taarifa maridhawa..

Though naona uzi unakosa wachangiaji kwasababu ya hii .. fita ni fita muraaa...!!

Mkuu waliosema Tanzania kuna njaa sasa naamini ni waongo maana sikujua kabisa kama tunao wafanyabiashara wakubwa ambao wanauza unga mwingi Tanzania. Tuna unga Chapa Manji, Chapa Gwajima na Unga chapa Mbowe halafu watu waseme tuna njaa labda njaa ya mchele.
 
Mi sijawahi fika Tunduma mpakani so nina swali Mr. Pascal Mayalla
Hicho kituo kinajengwa upande wa Tanzania tu?, Je vipi kwa upande wa Zambia? Maana kule Rusumo walijenga pende zote za Tanzania na Rwanda.
 
Back
Top Bottom