Swali

TANMO

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2008
Posts
12,130
Reaction score
12,860
Wajameni naomba kuelimishwa, huyu mama amezindua hiyo Meli akiwa kama nani Serikalini? iwapo litatokea swala lolote juu ya hiyo meli, ni nani hasa atakuwa responsible? Je ni yeye au ni mume wake?

Naombeni mnifute ujinga..






Mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda Akizindua Meli ya Ocean Rig Poseidon ya Kampuni Ya Petrobas Ya Brazil Kwa Ajili Ya Kufanya Utafiti Wa Mafuta Katika Pwani ya Mtwara na Mafia. Uzinduzi Huo Ulifanyika Mji Wa Geoje, Korea Kusini. Picha Zote: Hilary Bujiku, Ofisi Ya Waziri Mkuu

Picha kwa hisani ya Mjengwa Blog.
 
hii nchi shamba la bibi
sijui kama serikali hii ina washuri
kama kwa FL iliwezekana kwenye kampeni na
hata sasa akienda wilayani au mkoa anapokelewa ka
kiongozi wa serikali USISHANGAE hata mwanae PM angeweza zindua
 
Serikali yetu inaendekeza sana mambo ya """"tangu leo mmekuwa mwili mmoja" ambayo baba wa taifa aliikataa kwa kumkalipia Mama Sitti Mwinyi alipoanza kuingilia mambo ya serikali......lakini sasa ndugu yangu...Baba hayupo tena (Mungu amlaze pahala pema Nyerere) kila mtu na mke wake wanasaidiana kuongoza nchi...." Kwa wale wanaojua hii lugha ya kabila moja wanasema "omwanshonzi mareju" hivyo usishangae siku moja Salma Kikwete anakabidhiwa kiti wakati mume wake kasafiri....
 
Mwisho wataanza kuingia bungeni na kulamba posho sasa,serikari imeishakuwa ya familia zao,watoto,mashangazi,bibi zao nk.
 
hii nchi shamba la bibi
sijui kama serikali hii ina washuri
kama kwa FL iliwezekana kwenye kampeni na
hata sasa akienda wilayani au mkoa anapokelewa ka
kiongozi wa serikali USISHANGAE hata mwanae PM angeweza zindua

Uko sahihi kaka hii nchi isha potezwa?? who is who ???
 
Usisahau mkuu, kwa Tanzania mtu akiwa kiongozi serikalini basi familia yake yote ni viongozi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…