Swali, Umbea hustawisha mapenzi?(Ndiio au Hapana)

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,536
51,241
Assume umerudi job umechoka na mihangahiko ya town ile umekaa tu sitting room ghafla anakuja mkeo au mpenzi wako anakusogelea karibu na Sikio kwa Sauti ya chini anakuuliza "umesikia lililo mkuta mshana jr".

Tufanye mshana ni jiran yenu na labda kuna jambo la aibu kalifanya ambalo shemeji yetu kaliona sasa inawezekana si kitu ambacho Ulitaka kusikia kwa muda ule,

Lakini hey Inaonekana itakuwa ni habari nzuri kwako, huku ukihisi kuchangamka moyo na akili unaamua kumjibu mkeo "kwani mshana kafanyaje" umeona mambo hayo!? Mkeo/mpenzio anaamua kukupa a-z ya yaliyomkuta mshana anakueleza jambo baya na wewe unahisi moyo wako ume tuli, UMEFURAHI EEH.

Au sasa umekaa bar na washikaji wako wa kiume, anapita demu wa kuitwa Niffah, mmoja wa marafiki zako anaanza kukushukia nondo na mengi tu kumuhusu @Niffah kwamba yupo hivi na hivi mabaya yake haya na haya, unaporudi home na wewe unamsimulia kuhusu uliyoskia kwa mshkaj wako, mkeo naye pengine anaongezeA aliyoyaskia saloon kuhusu Niffah.

Tabia hii sio nyinyi tu peke yenu ni tabia ya KAWAIDA KABISA KWA WANANDOA NA WAPENZI Wengi, tunapenda kuongelea mambo ya watu wengine ili tu kufurahisha nafsi zetu.

Kwa lugha nyepesi na sahihi nyinyi ni WAMBEA
Sasa wanasaikolojia wanadai watu walio kwenye mahusiano hupenda kufanya hivi kwa kuwa inawafanya WAPENZI ku bond na ni tabia inayojenga afya ya akili, kusikiliza mikasa na visa vya watu kunasisimua.

Ni ukweli usiopingika kuwa hatupendi kuitwa WAMBEA sababu tu ya tafsiri halisi ya hili neno umbea kamusi ya kiswahili inatafsiri kuwa ni tabia ya KUTOA taarifa bila kuulizwa, udakuzi uchongeaji, kilimilimi.. Hivyo neno umbea limekaa vibaya hivi.

Ni makosa kuwa WAMBEA mbele ya WAPENZI wetu?
UPI muda sahihi wa kufanya umbea?

Kila umbea unahohisi utamfurahisha mpenzio ni muhimu kumwambia au Yapo ambayo ya kuficha?

Nini mtazamo wako ni kweli umbea unanogesha penzi.
 
Huo sio umbea hiyo ni updating ya habari za mtaani
 
Umbea hapo umekujaje? Maana hizo ni updates za kitaani.
Hapana sio kweli huo ndio umbea
Inawezekana wewe na MO11 MNAJIFANYA HAMJUI MAANA YA UMBEA LAKINI NIMESHAISEMA KAMA NILIVOICHUKUA KUTOKA KWENYE KAMUSI YA KISWAHILI YA MWANA 1998 TOLEO NAMBA MBILI
 
Ni mbaya sana... ukiona au kukuta kitu cha mtu unayemjua au kujuana unakausha.. au unaweza simulia bila kumtaja muhusika moja kwa moja..
 
Back
Top Bottom