Swali? Ukianza upya elimu ya msingi ile ya juu inafutika?

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,675
40,926
Kuna hili swali limekua likinitatiza sana wakuu, nahitaji majibu yenu!

Mfano nikaamua kwamba nianze upya elimu ya msingi! Nikafanya mtihani nikafaulu!

Inamaana kwamba elimu yangu ya o-; a level na degree vitakua vimefutika automatically!

Au nitakua tu na cheti kipya cha elimu ya msingi lakini vingine vinabaki kua halali?

Asanteni.
 
kwa jinsi ninavyokuona kwenye avarta yako, wewe ukianza upya shule ya msingi, na akili yako itaanza upya tena
 
Unaongelea kubadilika kwa vyeti au elimu uliyokuwa nayo kichwani tayari? Cheti ni utambulisho wa knowledge uliyo weka kwenye brain yako katika ngazi tofauti. Kama kurudia primary education kunaondoa ile elimu ya kwanza ya primary na kuporomosha nyingine juu yake kama ukuta wa tofali, jibu tayari unalo.
 
Na Mimi naomba niongeze swali katika hilo.....
Kuna mshikaji alimaliza kidato cha sita enzi hizo na kupata div 3 ya points 14 kwa maana ya D E E na kwa vigezo vya wakati alifanikiwa kijiunga na chuo kikuu kuchukua shahada yake, sasa kahitimu bahat mbaya iyo shahada haina ajira anafikilia kurudi chuoni tena kusomea shahada nyingine, kutokana na matokeo yake ya kidato cha sita wakati ule ana kosa sifa za kuchukua shahada kwani sasa wanataka walau mtu uwe na D mbili, kwa maana hiyo atatakiwa kurudia kidato cha sita swali je degree yake ya awali itaendelea kutambulika?
 
Degree yake ya mwanzo inatambulika, ila akirudia form 6 atapata vyeti viwili sasa complications huja pale anapoambiwa awasilishe cheti chake alipohitimu Mara ya kwanza, fine atarudia na pengine atafaulu kupata degree nyingine ila kila atakapokwenda atalazimika kubeba vyeti vyote viwili na kutoa ufafanuzi panapohitaji ufafanuzi
 
Unaongelea kubadilika kwa vyeti au elimu uliyokuwa nayo kichwani tayari? Cheti ni utambulisho wa knowledge uliyo weka kwenye brain yako katika ngazi tofauti. Kama kurudia primary education kunaondoa ile elimu ya kwanza ya primary na kuporomosha nyingine juu yake kama ukuta wa tofali, jibu tayari unalo.
Nilikua namaanisha kwamba kwa mfano nikaanza shule ya msingi upya? Ina maana vile vyeti vingine vyote vinakua havitambuliki? Maana sasa labda cheti ya darasa la saba kitasomeka 2016 na labda degree yangu itasomeka 2005 maybe!
 
sera ya elimu na mafunzo ya ufundi inakataza mtu mwenye zaidi ya 12 kuandikishwa shule ya msingi namaanisha darasa la kwanza. ukipita umri huo zamani ilikuwa unasoma Memkwa, au elimu ya watu wazima.
 
Back
Top Bottom