Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,273
- 21,455
Dr. KIngwangalla, nakupa pongezi kwa spidi uliyoanza nayo kazi kama Naibu Waziri, lakini ningependa kukuuliza swali ndogo kama reality check.
Juzi hapa panapo saa 1:32 asubuhi ulifunga geti katika ofisi ya Wizara ya Afya kwa sababu ya kutaka kuwakamata wafanyakazi "wavivu"
Dr Kingwangalla, ningependa nifanye tathmini ya maisha yako ya kazi na yale ya mfanya kazi wao wa kawaida ambaye ulimfungia geti kwa kumhukumu kwamba yeye ni "mvivu".
Nitachukulia kwamba wewe unafika ofisini saa moja na nusu aubuhi, na moja kwa moja unaenda ofisini kwako. Unakuta meza yako imepangwa vizuri na msaidizi wako binafsi anakuja na orodha ya shughuli za siku hiyo.
Ukimaliza kazi utamwambia katibu muhtasi wako amwambie dereva wako uko tayari kwenda nyumbani. Utakuta dereva wako amepaki gari anakusubiri, gari ikiwa inaunguruma na imewashwa kiyoyozi ili wewe mheshimiwa usisikie joto katika safari ya kurudi nyumbani. Kuna mtu atakubebea brief case yako kupeleka kwenye gari, na ukifika kwenye gari yako utafunguliwa mlango wa gari. Utakaa na kukuta magazeti pembeni mwa kiti chako ili usome kupitisha muda wakati wa safari kuelekea nyumbani, ukiwa umekaa kwa kujitanua kwa starehe na bila kubanwabanwa, ukisoma magazeti.
Ukifika nyumbani mnamo saa kumi na mbili jioni utakaribishwa vizuri, na labda kupewa kinywaji baridi. Utavua nguo za siku hiyo na kuzitupia mahali ili zifuliwe na mfanyakazi. Utaenda kuoga na kukuta kila kitu kimeandaliwa, mataulo safi nk.Ukimaliza kuoga utakuta nguo za kubadili zimeandaliwa na kupasiwa.
Kisha chakula kitawekwa mezani kwa ajili yako, na unachotakiwa kufanya ni kujivuta tu mezani na kula. Ukimaliza kula utaondoka na yupo mtu atakayehangaika kuondoa vyombo mezani na kuviosha. Hutajali juu ya watoto wako wadogo wanaosoma, kama unao, kama wamefanya homework, kwa kuwa kuna mtu yupo kwa ajili ya kuwasaidia. Utaangalia saa na kusema labda ni saa tatu usiku umechoka sana na kazi za siku unakwenda kulala.
Asubuhi utaamka na kukuta kila kitu kimeandaliwa ili uoge, na kuvaa; nguo zinepigwa pasi nk. Utakuta kuna mtu alishaamka asubuhi sana kukutengenezea kifungua kinywa. Ukimaliza, kama kawaida, utaacha vyombo mezani na dereva wako ataingia ndani kukubebea brief case na kuiweka kwenye gari muazne safari ya kwenda kazini, maana leo umemwambia muhawi kuna sababu maalumu,
Na kweli derava amejitahidi na kuwahi kukufikisha kazini ndani ya gari ya kiyoyozi uliyopewa na serikali, na mara moja unakimbia kwenda kufunga geti maana saa inakuambia ni saa 1.30 asubuhi.
Sasa kuna yule mfanyakazi wako mwingine hapo wizarani. Ni saa kumi na moja na nusu anatakiwa arudi nyumbani. Anakumbuka mwanaye aliyeko shule ameomba amnunulie vifaa kadhaa vya shule, hivyo lazima akimbie pale Imalaseko kabla hawajafunga. Anatembea kwa mguu hadi kufika pale na kununua vifaa, na ndipo anaeekea kitua cha basi posta mpya, ambako anakutana na patashika ya usafiri wa daladala. Baada ya kusubiri kwa saa nzima hatimaye anafanikiwa kujibana ndani ya daladala huku ameshika mfuko wa bidhaa zake kwa nguvu asije akaibiwa. Inatokea kwamba huyu mfanyakzai wala hakai mbali sana na unapokaa wewe.
Safari ya kurudi nyumbani ndani ya dala dala ukitia ndani na foleni na kushusha na kupakia abiria inamchukua karibu masaa mawili, na anasema leo ni afadhali. Hatimaye mnamo muda wa saa moja na nusu usiku anafika kituo chake cha nyumbani. Anatembea kwa miguu kutoka kituo cha basi hadi nyumbai na akifika nyumbani anasailiwa na kila aina ya mahitaji ya watoto. Mboga imeiva, ila inahitaji kuungwa. Anasaidia na kumalizia matayarisho ya mlo wa usiku. Baada ya mlo kuna suala la usafi, kuosha vyombo nk. Kisha suala la kusaidia watoto na homework. Kisha kuhakikisha watoto wana kila kitu kinachohitajika shule kesho yake.Kisha kuhakikisha watoto wote wamelala. Anaangalia muda, anakuta ni saa sita usiku tayari, ndipo anapata muda wa kwenda kuoga ili alale apumzike. Anapoingia kitandani kulala ni saa saba usiku.
Saa kumi na nusu alfajiri, baada ya kulkala kwa masaa matatu na nusu, anaamka ili kuanza matayarisho ya watoto kwenda shule. Saa kumi na moja na nusu anawasindikiza watoto hadi kituo cha basi la shule. Saa kumi na mbili asubuhi na yeye anayaanza kusubiri usafiri wake wa kwenda kazini. Kila basi linalopita linakuwa limejaa, hivyo anaamua ni bora alipe nauli mara mbili ili "azungushwe" na basi na kuweza kuwahi kazini. Saa kumi na mbili na nusu anapata kiti na kukaa ndani ya daladala tayari kwa safari ya kwenda kazini. Tatizo ni kwamba tayari foleni barabarani imeanza. Dereva wa daladala anakatisha na kutanua na hatimaye saa moja na nusu kamili anafikisha abiria wake posta mpya. Huyu mfanya kazi wako anashukuru kwamba angalau leo amewahi. Anatembea hadi kufika ofisini, ambapo anafika getini saa moja na dakika arobaini, na anaambiwa na walinzi Naibu Waziri amefunga geti.
Baadaye anasoma katika gazeti Naibu wake Waziri akimpachika jina kuwa yeye ni mvivu.
Hivyo swali kwako Mheshimiwa Kingwangallah, ni kwamba, hivi umewahi kukaa na wafanyakazi wa Wizara yako angalau ukawauliza ni jinsi gani uongozi wa Wizara unaweza kuwasaidia katika kuwahi kufika kazini na kurudi nyumbani, kabla hujawaita wavivu?