Kwa zama hizi ambazo mataifa makubwa yanatazamana kama majogoo yanayotaka kupigana sidhani kama kuna taifa linaloweza kutuuzia silaha ambazo ni zao la teknolojia yake mpya kabisa. Tunauziwa makapi halafu tunayafanyia maonesho, hakika tumeistaajabisha dunia. Hivi lengo lilikuwa ni nini hasa? muungano unadumishwa kwa siraha? Mbona tunafanya mambo bila kufikiri? Hoja sasa zinajibiwa kwa vioja. walituambia serikali tatu itapelekea jeshi kuasi, jana wakatuonyesha siraha zitakazo tumiwa na jeshi katika uasi huo, hovyo kabisa. Eti jeshi lipo fiti kulinda muungano, wapi uliona muungano unalindwa na jeshi? kama sio udikteta ni nini? Wekezeni kwenye elimu baada ya miaka 30 tuwe na vijana angalau wanaoweza kuunda siraha ili baada ya miaka 40 tufanye maonesho ya siraha zetu wenyewe hata kama ni low quality lakin ni zetu! na dunia nzima tutaiambia hivyo! Yes, ni zetu! Sisemi tusinunue siraha ila basi tuandae mazingira ya kuwa na vyetu.