punainen-red
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 1,731
- 450
Hivi huyu hussein na yule mama aliyekuwa anauza wanyama pale ikulu miaka ya nyuma wana uhusiano wowote?! Anakumbushia alichoona wazazi wanafanya!! Ndege ya jeshi la nje haiwezi kutua nchini bila jeshi letu/wizara ya ulinzi kuhusika. Huyu mtu huyu ni JANGA KWA TAIFA, msijesema hatukujua...Kwa kuleta hii kesi mahakamani, serikali imekiri kuwa kuna ndege iliingia nchini aidha kwa kufuata sheria au kinyume cha sheria. Lakini ingekuwa ni ndege ya kiraia hilo lingekuwa kashfa tosha lakini kuwa ni ndege ya kijeshi ni kashfa mabayo kama waandishi wetu wangekuwa na ujasiri wangetaka maelezo toka JWTZ.. muone watu wanavyoweza kujiuma uma meno!! Hii ni kashfa kubwa kweli ambayo Dr. Hussein Mwinyi anatakiwa aitolee maelezo.
hawa jamaa wameiba sasa wameamua kuamisha nchi.
hapa hakuna siri wote wanajua kuanzia mkuu wa kaya
mbona tausi wetu waliuzwa wakati wa utawala wa mzee rukusa
waziwazi .
hii nchi nilishasema mwanzo jk anapotosha na huyo mzee rukusa
mke usije kuta ndiye muusika mkuu maana mama anawataja wa kila
aina huko arabuni.
swali sio hiyo ndege kutumia tanzania ila ilitokaje huko QATAR bila sekarali ya
Qatar kujua kwamba wana dege lao limeelekea bongo?
ni wazi kulikuwa na mawasiliano ila tu mission imeingia mchanga,
isitoshe unaweza kuta hiyo ndege imeleta mzigo hapa ambao hatujui pia au kuondoka na vitu
vingi zaidi ya hao wanyama.
jk atoke IS TOO MUCH NOW!!!!!!!!!
Sina shaka kwamba ndege hiyo ilifuata taratibu za kuingia nchini, hivyo ilikuwa pale kihalali. Tatizo naloliona ni aliyetoa kibali hicho cha ndege kubwa ya kijeshi kama hiyo kuingia na kutua nchini alizingatia vigezo vipi? kwa kuwa alipaswa kutilia shaka maombi hayo na kuinyima kibali kama kweli anafanya kazi yake kwa kuzingatia sheria, utaratibu na common sense pia.Kwa kuwa mtoa kibali hakutumia common sense ana wajibu wa kutujibu watanzania kwa nini hakutumia common sense, na tuanzie hapo kuwakamata wahusika wote. Pili, wizara yetu ya mambo ya nje isikae kimya kama ilivyokaa kimya kuhusu suala hili, huu ni mgogoro wa kidiplomasia pia, hivyo lazima itoe kauli na kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kuhitaji twiga hao warudishwe nchini mara moja, na waarabu wote waliokodishwa viunga vya wanyama loliondo mikataba yao isitishwe mara moja na wote wafukuzwe nchini mara moja. Kama hatua zote hizi hazichukuliwi basi kwa kutumia common sense nitakuwa sina budi kuamini kwamba viongozi wajuu wa serikali ni wahusika wakubwa wa wizi huu, na wale ambao wamefikishwa mahakamani ni dagaa tu, kambale wapo nje huru.
Kila kitu kinajibika ila naona tunajadili newspaper article ambo ilikuwa poorly written
Hakuna basic facts na imekuwa kama mtego vile wa waandishi kutaka kupima akili za wana JF
Unless watu wa WANYAMAPORI na UTALIII na JESHI LA POLISI watoe statement lakini hii kujadili newspaper article iliyoandikwa na huyu mwandishi anayeoonekana kama vile anaandika news kwenye gazeti la Primary school is just beyond ridiculous
sasa mjanadili facts au poorly written newspaper article isiyo na fact yoyote?
Poorly written article - what exactly do you mean ndugu SlidingRoof? Kwamba ukisoma hiyo article hauoni/huwelewi ni kitu gani kimeandikwa?!!! Hivi inawezekana kweli hii article haina facts?
Mwandishi ametaja kuwa ndege ni ya kijeshi toka Qartar, imetuwa KIA, ametaja idadi na aina ya wanyama waliosafirishwa pamoja na thamani, pia ameeleza kuhusu kesi iliyofunguliwa dhidi ya watuhimiwa wa sakata hilo (including nchi walikotoka). Sasa wewe unataka facts gani?
Kusema kwamba watu wanajadili poorely written article your are in my view missing the point. Nijuavyo mimi hapa jamvini watu wanajadili hoja kwa maana ya contents na siyo style. Nashauri usome tena hii article and this time around try to be more attentive.
je nikweli ndege ya jeshi iliagizwa nchini kwa nguvu ipi?mana huwezi tua katika nchi yoyote duniani na kutekeleza uhalifu pasipokuwepo mkono wa mwenye nchi. Je ni kweli wale watuhumiwa ndio hasa waliokula njama za kutorosha nyara izo pasipokuwepo watu wazito {vigogo} nyuma yao? Mi nadhani kuna siri ambayo ipo Nyuma ya hawa wanaotuhumiwa.