Swali la wasiwasi: Je, mikutano ya kisiasa itakaporuhusiwa Wapinzani watapata Nyomi kama la Dr Bashiru na Polepole?

Hujasikia kila bendera za CHADEMA zikipandishwa DC anaamuru ziteremshwe? Kama unajidanganya kuwa CCM inapendwa kivile unajidanganya. Bila msaada was dola CCM ni wepesi kuliko karatasi!

Tissues mkuu wacha paper
 
Umehakikishiwa uchaguzi utakuwa huru na wa haki acha kulialia kama Kigwangala!

Hiyo ni danganya toto tu kutoka kwa Binadamu kama wewe /mimi na wengine ,ukifika huo wakati wa Uchaguzi inafuatwa Sheria (Mfumo) ambao sio Rafiki sababu hautoi Haki ktk Mizania ya kuchagua na kuchaguliwa.
 
Najiuliza tu kwa sababu kwa sasa wananchi wengi wameshavisahau vyama vya upinzani ukiondoa kule Zanzibar, Mbeya mjini, Iringa mjini na Tarime.

Ndio najiuliza mikutano itakapofunguliwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu vyama vya upinzani vitapata watu au watalazimika kuwabeba kwa malori kama wafanyavyo Cuf na Chadema.

Nipo hapa Ludewa ambako Masanja Mkandamizaji atagombea ubunge kupitia CCM, kiukweli sijaona hata bendera moja ya Chadema ikipepea wilaya nzima.

Maendeleo hayana vyama!
You must be kidding

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeye ndio kinara wa kunajisi uchaguzi hapa nchini. Hakuna mtu anayejitambua atashiriki uchaguzi wa kishenzi bila tume huru vya uchaguzi fullstop.
Haya pingeni wala msichukue fomu ili ccm ipite bila kupingwa. Fullstop
 
Kwa kweli kwa dozi kila kona ya miaka minne hapa kazi, dona kantri, nchi ya viwanda, mabeberu, nchi inaibiwa, na tunatekeleza Stigler na SGR basi sie sasa tunaweza tabiri nini kinatasemwa kwenye hiyo mikutano ya CCM. Nafikiri tutaenda kuwasikiliza wengine kama wana ofa ya maana kushinda hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kimsingi ccm haiwezi ushindani, njia pekee wanayotegemea kupata ushindi ni huo ushindi wa mezani.
Mkigoma kujiandikisha na pia kuchukua fomu, au mkifanya madudu kwenye ujazaji mnataka kubebwa tu?? Kama kiongozi hajui hata kuijaza fomu, wa nini kumchagua?
 
Mkigoma kujiandikisha na pia kuchukua fomu, au mkifanya madudu kwenye ujazaji mnataka kubebwa tu?? Kama kiongozi hajui hata kuijaza fomu, wa nini kumchagua?

Fomu gani hizo za maajabu ambazo watu hawawezi kujaza? Hakuna mpinzani anataka kubebwa, ccm ndio wanategemea kubebwa. Wapinzani wanataka uchaguzi wa haki tu. Hatuna tatizo la ccm kushinda, bali hatuko tayari ccm kutangazwa washindi bila kushinda.

Tumeona kwa macho yetu kwenye chaguzi chini ya awamu hii kukifanyika ukatili na uhayawani wa wazi ili ccm watangazwe washindi. Na matendo yote hayo maovu yanafanyika kwa uratibu wa jeshi la polisi, na tume ya uchaguzi wanatangaza washindi fake. Ni mtu mjinga, asiyejitambua na anayefaidika na hizo chaguzi za kishenzi, atapoteza muda wake kushiriki huo uhuni wa kitoto.
 
Back
Top Bottom