Swali la wasiwasi: Je, mikutano ya kisiasa itakaporuhusiwa Wapinzani watapata Nyomi kama la Dr Bashiru na Polepole?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Messages
26,438
Points
2,000

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined May 27, 2014
26,438 2,000
Najiuliza tu kwa sababu kwa sasa wananchi wengi wameshavisahau vyama vya upinzani ukiondoa kule Zanzibar, Mbeya mjini, Iringa mjini na Tarime.

Ndio najiuliza mikutano itakapofunguliwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu vyama vya upinzani vitapata watu au watalazimika kuwabeba kwa malori kama wafanyavyo Cuf na Chadema.

Nipo hapa Ludewa ambako Masanja Mkandamizaji atagombea ubunge kupitia CCM, kiukweli sijaona hata bendera moja ya Chadema ikipepea wilaya nzima.

Maendeleo hayana vyama!
 

Ngorunde

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2006
Messages
1,708
Points
2,000

Ngorunde

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2006
1,708 2,000
Kati ya makosa yaliyofanywa na CCM, kubwa ni hili la kuzuia mikutano ya vyama vya upinzani.

Kitendo cha kuwaziba mdomo kitakuwa kimejenga shauku kubwa ya wananchi kuwasikia tena viongozi wa upinzani na hoja mbadala.
Hali hiyo itavuta watu wengi sana kwenye mikutano yao.

Tusubiri kipenga!
 

Lord eyes

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2018
Messages
7,045
Points
1,995

Lord eyes

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2018
7,045 1,995
Tume wachia tume na dola ni ya kwenu mtawale mpaka Basi huwenda kuna watu wametumwa duniani kutawala hata Kama hawana maarifa ya uongozi
 

mangatara

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2012
Messages
13,986
Points
2,000

mangatara

JF-Expert Member
Joined Jul 6, 2012
13,986 2,000
Sio vyema kuleta utabiri wa kichawi mapema. Tusubiri kipenga na ahadi ya uhuru aliyoitoa mkuu wa kaya iwepo halafu ndo tuone. Nnani atakodi malori na Nnani watatembea km 50 kwa miguu kwenda kumsikiliza. October is jus near. Siku hazigandi
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
26,539
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
26,539 2,000
Sio vyema kuleta utabiri wa kichawi mapema. Tusubiri kipenga na ahadi ya uhuru aliyoitoa mkuu wa kaya iwepo halafu ndo tuone. Nnani atakodi malori na Nnani watatembea km 50 kwa miguu kwenda kumsikiliza. October is jus near. Siku hazigandi
Yeye ndio kinara wa kunajisi uchaguzi hapa nchini. Hakuna mtu anayejitambua atashiriki uchaguzi wa kishenzi bila tume huru vya uchaguzi fullstop.
 

Forum statistics

Threads 1,391,831
Members 528,475
Posts 34,090,811
Top