Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,739
- 40,864
Ni wazi kuwa siyo watu wote wanaopenda Magufuli afanikiwe katika ajenda zake za kisiasa; kwamba hawapendi baadhi ya mambo yaende vizuri kiasi cha kumfanya Magufuli ajisimike zaidi katika kutimiza ahadi zake za Uchaguzi. Watu hawa kwa mfano wanaweza wasiwe mashabiki wa Mahakama Maalum ya Kushughulikia Kesi za Uhujumu Uchumi na Ufisadi; au wanaweza pia wasiwe mashabiki wa dhana nzima ya Elimu ya Bure au kubana matumizi yasiyo ya lazima.
Wengine wanaweza kujibanza kama ni 'wakosoaji' lakini kiukweli siyo uokosoaji bali ukwamishaji. Wanataka Magufuli akwame. Kwanini? Wanataka ahadi za uchaguzi zisifanikiwe kwanini? Inawezekana wana sababu za kweli na za msingi - lakini ni bora waseme hivyo wazi.
Mtangazaji Maarufu wa Radio Marekani Bw. Rush Limbaugh (role model wangu kwa kweli) aliposhinda Obama alisema wazi kuwa "I hope he fails" na watu wakamjia juu sana kwanini anataka Rais ashindwe. Ukweli ni kuwa alikuwa anasema hivyo kwa sababu aliamini sera na mipango ya Obama ilikuwa inatishia mafanikio ya sera za wahafidhina wa Marekani. Kwamba, alitaka sera za Obama zishindwe kwa sababu hakuwa anazipenda. Sasa alikuwa wazi na hadi leo hii hakujificha katika hilo na watu wengi baadaye wamekuja kukubaliana naye.
Bila ya shaka naye Obama alikuwa na watetezi wake ambao walitaka afanikiwe na wamefurahia kufanikiwa kwa sera zake mbalimbali - kuhalalisha ndoa za mashoga, kupunguza makali ya jeshi la Marekani, kuwa na sera kali za kulinda mazingira (hasa masuala ya uchimbaji mafuta), kufunga kambi ya Guantanamo n.k.
Sasa inawezekana wapo ambao wanataka Magufuli ashindwe kweli; lakini ni vizuri waseme wazi kuwa anataka kushindwa na waseme ni kwanini ashindwe. NI muhimu kuhoji na kujiuliza kama kweli wote wanaojitokeza kumpinga Magufuli au utekelezaji wa ahadi zake wanafanya hivyo kwa nia njema au wana kitu kingine kinawasukuma. Siyo kila anayekosoa au kumpinga Magufuli ni kwa sababu anawatakia Watanzania mema. Na wengine wanaweza kuwa na sauti kweli kweli.
Si inasemwa mwisho wa uchaguzi mmoja ni mwanzo wa maandalizi ya uchaguzi mwingine? Siyo kwamba ni kweli wote walioonekana na nyuso za furaha walikuwa wanafurahia kweli ushindi wa Magufuli? Wengine ilibidi wawe na nyuso za furaha... sasa wangefanyaje?