Swali kwa wenye vyama

Swali kwa wenye vyama

md4doctor2000

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2012
Posts
736
Reaction score
315
Wewe ni mwanachama wa chama fulani, umeamua kwa hiari yako (au kwa kushawishiwa) kukihama chama chako na kuhamia chama kingine, kwanini haurudishi kadi (ya chama unachokihama) kwenye chama ulichokuwa (ambao ndio wenye kadi) bali unarudisha kadi katika chama unachohamia?
 
Babu alipoulizwa kwanini hajarudisha kadi ya CCM alisema "akiba haiozi"...
 
Wewe ni mwanachama wa chama fulani, umeamua kwa hiari yako (au kwa kushawishiwa) kukihama chama chako na kuhamia chama kingine, kwanini haurudishi kadi (ya chama unachokihama) kwenye chama ulichokuwa (ambao ndio wenye kadi) bali unarudisha kadi katika chama unachohamia?

Naona safu yako ya mwili, nafsi na roho hazishirikiane vema...............tunafanya siasa kwa mwongozo wa sheria, sasa wapi kuna sheria ya kurudisha kadi ukihama chama..............nakusaidia bila hela: sheria inasema ukipewa kadi ya chama kingine, ama ukihamia chama kingine automatically unakuwa umejifuta uanachama wa chama chako cha mwanzo............nenda lumumba kachukue posho yako ya wikiend leo umeandika thread nzuri sana, nape kaipenda hii!!!!!
 
kila mwenye mawazo tofauti CDM anapata posho. nawe kapate ruzuku.
 
Binafsi naona ni jambo la busara kuiacha kadi ya chama cha awali katika ofisi za chama hicho ili iwasidie kutunza kumbukumbu za wanachama waliohama. Nakumbuka hata mwalimu Nyerere wakati akina mzee Malechela na Lowassa pamoja na watoa maamuzi wa CCM walipotaka kumchanganyia habari alitaka kuirudisha kadi ya CCM kwa CCM. Na kuwatamkia kuwa CCM si mama wala baba. Pamoja na kwamba Nyerere si msaafu lakini mantiki ya kufanya hovyo iko wazi

Hawa wanaorudisha kadi ya chama cha awali kwenye ofisi za chama kipya ni just show off kuna dalili zote za kuwa wachumia tumbo. Kama ni sherehe ya kuwapokea kwenye vyama vipya kwa nini wasisherekehe kwa kupewa kadi za chama hicho kipya? Ninachokiamini mimi kama mtu si mamluki au mpenda uongozi kupindukia ( power monger) si rahisi kuhama chama kimoja na kwenda kingine kila mara.

Kwa vile tulikuwa na chama kimoja hapo nyuma na baada ya vyama vingi kuruhusiwa basi tunategemea watu wahame toka CCM kwenda vyama vya upinzani na baada ya hapo tushuhudie watu wakiwa na misimamo thabiti. Uamuzi wa kuhama CCM ukaenda upinzani mara umerudi CCM siyo uamuzi wenye tija ndani yake. Kushindwa kwenye uchaguzi katika chama fulani na kukimbilia kingine huo ndo upower monger au ni kukurupuka kujiunga na chama fulani bila kukifahamu vizuri matokeo yake ni kuhamahama na mtu wa namna hiyo hafai kuwa kiongozi.

Chama ni taasisi kama wewe ni kiongozi mzuri kwa nini usibaki huko na kuwashawishi wanachama wenzio kudai mabadiliko unayofikiri ni lazima yafanyike? Huko unakohamia umekaa lini na kuelewa kama hawana matatizo zaidi ya unakotoka?
 
Kadi ni mali ya chama husika,kwa hiyo ni kosa kurudisha mali ya watu kwa watu wengine..hii ya kurudisha kadi ya chama unachohama kwa chama unachohamia ni upumbavu tu usio na maana..HII YOTE NI KWA SABABU YA CCM NA CHADEMA KUTAKA KUONYESHA KADI HIZO KWENYE VYOMBO VYA HABARI,KWA SABABU WAKIWARUDISHIA WENYE MALI(KULE WANAKOTOKA)HAZITAONEKANA KWENYE TV
 
Back
Top Bottom