Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,267
- 23,203
Kwa sasa wananchi wengi wamejawa hofu, mashaka na sintofahamu kubwa kutokama na utendaji usioridhisha wa Jeshi letu la Polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama. Katika kipindi cha karibuni polisi wetu wameonesha upungufu mkubwa kimaadili katika utoaji wa haki sawa bila upendeleo kihali, kimali, kidini, kiitikadi, kirangi, kikabila wala kijinsia.
Kwa sababu hii ninapatwa na wasi wasi kuhusu hasa wale polisi ambao kwa namna moja ama nyingine wameonekana kushindwa kutekeleza wajibu wao kwa weledi kama walivyoapa. Pia dalili za wazi wazi za upendeleo zimeonekana pale Jeshi la Polisi linapotumika kuwadhibiti raia ambao wanatoa kauli au matamshi ya kuikosoa hii serikali ya awamu ya tano.
Je yawezekana ndani ya Jeshi hili wapo ambao kwa matendo yao wanatupa mashaka kama kweli walipitia mafunzo kama wenzao? Msingi wa wasi wasi huo ni hawa hapa chini, je baada ya uwepo wao kwa mwamvuli wa chama kupigwa marufuku, kwa sasa wako wako wapi?