Swali kwa wapendanao..

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,189
39,954
  • Mke na mume walikuwa wakirudi nyumbani mida ya saa 2 usiku kutoka katika miangaiko yao ya kutafuta kipato.Walipofika nyumbani wakahisi nyumba yao imevamiwa, na ina mtu ndani kwa sababu mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani.
  • Mume akaanza kutindua ukuta karibu na mlango ili aweze kuufungua,pakapatikana tundu dogo la mkono kupenya.Basi mkewe akaomba amsaidie kufungua mlango.Wakati anaingiza mkono ndani ili afungue kitasa,yule mwizi aliyekuwemo mle ndani akaukata ule mkono kwa panga;yule mama alijikaza kisabuni bila kupiga kelele akautoa mkono wake taratiibu na kuuficha......akamwambia mumewe naye ajaribu kufungua kwani yeye amechoka.
  • Mumewe alipoingiza mkono ndani naye akafyekwa mkono....akapiga kelele za maumivu na kusema nimekatwa mkono.....basi na yule mkewe akamuambia nami pia nimekatwa mkono....kwa hiyo tumefanana.
  • Swali ni yupi alikuwa na mapenzi ya kweli kwa mwenzie?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom