Swali kwa waliomo kwenye ndoa

dad24

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2013
Posts
464
Reaction score
121
Habari wana MMU,ni matumaini yangu mu wazima wa afya njema kwa ambao hawako sawa mungu awajalie afya njema.....................................................

Turudi kwenye maada, imekuwa ndiyo kasumba ya sasa kwa waliomo kwenye ndoa kutosema mazuri ya huko na baadala yake wamekuwa wamekuwa wakisema mabaya tu mfano mzuri ni humu ndani threads nyingi zimekuwa za kusema machungu tu yanayopatikana huko manyanyaso,kutotendeana haki na mengine mengi lakini kwenye kiapo cha ndoa kuna sehemu inasema nitampenda na kumtunza kwenye shida na raha lakini mbona hizo raha mnazopata huko hamzisemi,shida tu ndiyo mnatujuza? swali:-

1.Mnataka kutuambia kuwa huko hakuna raha zaidi ya shida?

2.Kama zipo mbona hamleti thread za utamu wa ndoa ili tuwatamanie?

3.Je ni kugegeda/kugegedwa tu au kupata watoto ndiyo raha? na kama kugegeda na kuwa na watoto ndiyo raha wapo ambao tunagegeda/kugegedwa na tuna watoto lakini hatuko ndani ya ndoa......

Wakati huohuo mnakuja na thread za athari za kuchelwa kuoa/au kuolewa sasa hiyo morali ya kuoa au kuolewa inatoka wapi wakat nyie hamtuambii raha mnaleta matatizo tu tena usiombe mtu kaingia akakuta kwa moto akatoka hata kama ulikuwa kwenye process za kuingia utafunga break kwanza..............................

Hii inasababisha vijana wengi tujiwekee qualifications nyingi za kupata wenza mara ooh sitak umiza kichwa tumesahau kuwa huwezi kumpata ambaye haumizi kichwa unless ziwe zimepungua kidogo kichwani.
Haya karibuni mtwambie jamani..........
 
Mimi kila siku naisifia ndoa. Ndoa ni raha asikwambie mtu. Ndoa ya wapendanao ambao nafsi zao bila shuruti zimependana, zinaendana na zinakubaliana.

Hapa namaanisha mama atamuheshimu baba, na baba atampenda mama. Baba atalinda familia na kuhakikisha inafanikiwa, na mama ataitunza na kuipendezesha.

Hapa namaanisha mapungufu yanatatuliwa na wanandoa, na kuyageuza yawe mambo mazuri.

Hapa namaanisha hakuna siri za ex- boyfriends wala girlfriends. Hakuna siri ya ndugu wala bosi, hakuna siri ya safari wala mapato.

Hapa namaanisha kupanga mipango pamoja, kuset targets za kufanikiwa(projections), kupiga shule, kiufupi kufanikiwa pamoja kielimu, kipesa na kumcha Mungu.

Kila nikimuangalia mke wangu nahisi ni mimi. Unajisikiaje unapokuwa na pacha mwenzako ambaye mnashare kila kitu?

Ndoa raha sana.
 
hongera mkuu,ukishaanza kujiuliza hivyo ujue umekaribia kuoa:smile-big:
huwezi pata majibu ya moja kwa moja kwa sababu tuko tofauti na experiences zetu ziko tofauti..more worse ndoa haiji na manual ingawa siku hizi tumejitahidi na makitchen parties etc BUT in the end ni wewe utakavyolicheza na mwenzio.....
 
Nimekupata mkuu ndo useme kulingana na experience yako maana hata shida kila mtu huwa na za kwake
 

Anhaaaa! kumbe ndiyo raha zenyewe hizo mkuu mbona hazisemwi sana kuliko shida jamani?
 
walio bize na ndoa zao usidhani kama wapo hapa ,..hapa wamejaa watu na stress zao..me included...
So dont take MMU serious.
 
walio bize na ndoa zao usidhani kama wapo hapa ,..hapa wamejaa watu na stress zao..me included...
So dont take MMU serious.

Hahahaaaa... !!
 
walio bize na ndoa zao usidhani kama wapo hapa ,..hapa wamejaa watu na stress zao..me included...
So dont take MMU serious.
Hahahahaa...... so fun
 
Ni kama msiba na harusi mkuu

Harusi kwa waalikwa msiba kwa wote!!!!!!
Raha zako changamoto za kujadiliwa!!!!!
 
Ni kama msiba na harusi mkuu

Harusi kwa waalikwa msiba kwa wote!!!!!!
Raha zako changamoto za kujadiliwa!!!!!

Angalau kwenye harusi unajua nini kinaendelea hata ukija kuombwa mchango unatoa bila maswali wew unafikiri vijana wengi wakiume kw wakike wakiulizwa suala la ndoa sabab kubwa wanayokupa et tunajipanga huoni ni stail ya kukwepa baada ya kujua huko ni full mvurugano?
 
.................................................................
 
.................................................................

Dah! hapo kweli ni raha aisee.... eeeh muwe mnatuambia kama hivi jamani.........
 

....................................................
 
Kila kitu kina side mbili! utamu na uchungu, mwanzoni ndoa huwa tamu sana hiki nikipindi ambacho wanandoa huoneshana mahaba motomoto. Katika phase ya pili wanandoa huanza kuchokana na ndipo lawama, migogoro na kashfa huanza. Phase ya mwisho ni kuvumilia kasoro za mwenzi wako au kuachana.
 
Dah! hapo kweli ni raha aisee.... eeeh muwe mnatuambia kama hivi jamani.........


dad24

mkuu nikatika kubadilisha mawazo inatokea muda unaruhusu tunabadilisha uzoefu kila mmoja kwa anavyofahamu.

Nimeipenda sana hoja yako kiasi kwamba nikafunga breki kutolea maelezo ninayokumbananayo na ninayoyafaham.
 
Last edited by a moderator:

Hiyo phase ya kwanza ndo huwa haizungumziwi huwa wanaishia kusema tamu, huwa inakuwa sawa wapenzi wa kawaida wanaoanza mapenzi au hii inakuwa tofauti kidogo?
 
dad24

mkuu nikatika kubadilisha mawazo inatokea muda unaruhusu tunabadilisha uzoefu kila mmoja kwa anavyofahamu.

Nimeipenda sana hoja yako kiasi kwamba nikafunga breki kutolea maelezo ninayokumbananayo na ninayoyafaham.

Asante sana mkuu maelezo yako yameenda shule nina imani vijana tumepata kujua raha zilizomo na wengi huwa wanakimbilia huko kwa sababu wanajua watagegedana kwa uhuru bahati mbaya wanakuta ni zaidi ya kugegedana wanarudi wakilia huku waliingia kwa mbwembwe na kututisha wengine......
 
Umeonaeee!
Wengi hupost kwa kutafuta suluhisho la tatizo!
Sidhani kama itasound mtu kuja kumsifia mke/mmewe humu!

Ni kama msiba na harusi mkuu

Harusi kwa waalikwa msiba kwa wote!!!!!!
Raha zako changamoto za kujadiliwa!!!!!
 
Umeonaeee!
Wengi hupost kwa kutafuta suluhisho la tatizo!
Sidhani kama itasound mtu kuja kumsifia mke/mmewe humu!


Mashaxizo

mkuu mchango wako nimuhim, tupe uzoefu wako tunahitaji kujifunza kila wakati.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…