Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,272
- 21,448
Kabla hata Magufuli hajajitokeza kuchukua form za uraisi, na kabla hata JK hajamtaja Magufuli kuwa bulldozer, niliwahi kuandika humu JF kwamba Magufuli ni mchapakazi, lakini yuko kama bulldozer, anahitaji dereva makini.
Hivyo nilishangaa nilipoona JK kamwita Magufuli bulldozer, hata nikafikiri labda alisoma post yangu.
Sasa wakati CCM wakijiandaa na mkutano utakaoamua juu ya kupata mwenyekiti mpya wa CCM, ningependa kuwauliza swali; kama hata wao wamekubali na kutamka hadharani Magufuli ni bulldozer, dereva wa hilo bulldozer ni nani?
CCM wafikirie hii scenario; Bulldozer ni mashine nzuri tu ya kufanyia kazi, lakini fikiria bullldozer linawashwa, kutiwa gia, na kuliacha lijiendeshe jenyewe bila dereva katikati ya mji na watu! Ni wazi itakuwa pata shika na kasheshe ya mwaka! Hata wale wenye kumiliki bulldozer hilo watakuwa wakitimua mbio huku na kule wakati bulldozer likisonga mbele!
Ushauri umetolewa na watu wengi muhimu kwamba Tanzania tunapaswa sana kufikiria kutenganisha kofia ya raisi na mwenyekiti wa chama. CCM watafakari hili kwa makini. Ningeshauri CCM wawafikirie wale waliokuwa wagombea uraisi katika kuwa Mwenyekiti wa CCM, watu kama kina Prof. Mwandosya, Membe nk, na kumuacha bulldozer Magufuli na majukumu ya serikali. Ikiwezekana hili liwe jambo la kikatiba, sio CCM tu.