nyumbatatu
JF-Expert Member
- Jul 19, 2013
- 1,076
- 939
Habari za asubuhi wakuu!
Leo asubuhi mida ya mbili kasoro nikiwa nakatiza mataa ya Kamata kuelekea Gerezani/Kariakoo nimekutana na msafara wa kipekee wa polisi wakiwa kwenye Land cruisers Kama sita hivi zikiwa Nn polisi wasiopungua watano kwenye kila gari wakiwa wamejizatiti vilivyo huku wakiwa katika utayari wa kupambana.
Katikati ya msafara huo kuna basi dogo la magereza na kuna watu wawili tu wanaoonekana watuhumiwa huku wamezingirwa na askari magereza wenye silaha pia. Mbele kabisa kuna pikipiki ya trafiki(router) ikipiga king'ora!
Msafara huo ulipofika mataa ya Kamata ukitokea kKko/Ukonga ulilazimika kusimama (huku wakiwa wamelitenganisha basi la magereza na magari mengine kwa umbali usiopungua mita 25 kwa nyuma na mbele) kwakuwa kulikuwa na treni inatoka stesheni!
Hapo sasa mimi na raia wengine pamoja na wanafunzi wa shule za msingi tulikuwa tunavuka usawa wa basi hilo tukazuiwa wote tusisogee kulikaribia, jambo ambalo lilituacha kwenye mshangao na kutushawishi tuulizane bila kupata jawabu sahihi ni mhalifu wa aina gani kapewa escort yenye ulinzi mkubwa vile? Lakini kwa kuwa JamiiForums ni kisima cha habari nimeona nilete swali huku nijue.
NB: Sikuthubutu kujaribu kuchikua kapicha hata kwa kuibia kwa sababu mitutu ya bunduki ilikuwa imeelekezwa pande zote!( isitoshe pamoja na uncle Magu kubana bado maisha yana "ladha!")