Swali kuhusu maswala ya ajira

Swali kuhusu maswala ya ajira

a45

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
1,455
Reaction score
1,606
Wakuu habari kama kichwa kinavyo jieleza naomba wale wajuzi wa haya mambo na wahenga watusaidie swali liko hivi kwa miaka ya nyuma taifa Tanzania limepitia kipindi cha kuwa na rate kubwa ya watu ambao hawana ajira kama mwaka huu hali ilikuaje ?

Na je kuna mwaka kulikua na hali kama ya sasa watu kufanya interview kwa wingi kama tulio ushurudia mwaka huu mfano ktk ule usahili wa watu wa TRA na idadi inayohitajika ikawa ndogo kama mwaka huu ??

Wakuu naomba kuwasilisha
 
Ngoja waje mkuu ila miaka ya karibun hali ni mbaya zaid
 
  • Thanks
Reactions: a45
Haikuwahi kutokea......miaka ya kuanzia 2000's kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wahitimu wa level zote kuanzia shule ya msingi, sekondari, na vyuo. Na moja ya vitu vimeboost ongezeko hilo ni idadi ya watu waliodahiriwa vyuoni wakitokea form one bila kupitia form 5 na 6.

Kwa kifupi....short kati za kufikia elimu ya juu zimeongezeka plus mwamko wa watu kusoma na kuwa na satatus ya usomi vimechangia.

Kwa sasa hali ni mbaya sababu aina ya masomo yanayotolewa vyuoni ni mazuri ila wahitimu wake wana demand ndogo sana katika soko la ajara, yaani supply yao ni kubwa kuliko uhitaji. Mfano imagine, watu wanaohitimu uhasibu, mwisho wa siku katika kila taasisi kutokana na mabadiliko ya technology kama ya matumizi ya software za uhasibu kama tally ambazo huwa zinahitaji mtumiaji m'moja tu wa computer kufanya kazi za watu sita, hii imefanya idadi ya uhitaji wa wahasibu kushuka, na unaweza kuta bonge la taasisi kuna muhasibu mkuu m'moja tu na wasaidizi wake watatu tu labda. Sasa hao wapo kazini hadi watoke sio leo. Hapo lazima ajira zisiwapo.

Mbaya zaidi ajira zilizopo ni za toka niingie kwa maana zipo scarce. Only ajira zinazoweza chukua watu wengi kwa wakati m'moja ni za viwandani na zile zenye uhitaji wa wafanyakazi wanaoprovide physical labour force.......

So kujibu swali lako kwa mara nyingine ni kuwa swala la ajira kwasasa linaingia kuwa moja ya changamoto za kimaendeleo katika taifa letu. Na serikali wapo katika hali tete kulitatua kwa maana wamekwama kwa sasa. Therefore, serikali wanasafari ndefu kuja kusolve hilo tatizo kama wataendelea kutazama tu huu mfumo wa elimu lakini pia kama hawatakuja na mikakati mizuri ya kusapoti ukuaji wa sekta binafsi ambayo ndio kwa mujibu wa takwimu ndio inaongoza kwa kuajiri raia wengi sana.
 
  • Thanks
Reactions: a45
Back
Top Bottom