MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Ni wazi kabisa kua kuna baadhi ya viongozi wa serikali yetu ya awamu ya tano wanapingana na maamuzi ya serikali hii japo ni vigumu kulidhihirisha hilo wao wenyewe, ukitaka kulihakikisha hilo fuatilia tofauti ya kauli zao.
Kwanza mimi ningekua waziri wa kilimo,Chakula na uvuvi ningeachia ngazi bila kujadiliana na yeyote maana ni kweli maeneo mengi nchini kuna uhaba wa Chakula na njaa. Nisingeweza kufanya kazi huku nikona kuna familia zinalia na njaa, Dhamira yangu ingenisuta.Uwajibikaji unatoka moyoni na sio maneno ya mdomoni tu.
Najua naweza nitofautiane na wengi lakini ukilifanya hili kwa dhamira ya moyo wako kutokana na kuguswa na vilio vya wati juu ya tatizo basi unaweza kua kiongozi wa kwanza kujijengea heshima kubwa ndani na nje ya nchi.
Ikumbukwe kua wapo viongozi waliowahi kufanya hivyo lakini ilikua ni baada ya tuhuma na kunyooshewa vidole sana na umma.