Swali chokonozi: uchochezi ni upi hasa.

Swali chokonozi: uchochezi ni upi hasa.

TAWA

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
3,674
Reaction score
1,572
Wasalamu
Watu wanaofunguliwa mashtaka kwa makosa ya uchochezi wanazidi kuongezeka kadiri siku zinavyosogea. Wasi wasi wangu mimi wanaofunguliwa mashtaka haya ni watu wa aina ile ile na wa chama kile kile.
Sasa serikali ifike wakati itangaze matendo ambayo mtu akiyafanya yanakuwa yanaashiria uchochezi. Kwa sasa watu tunaanza kuogopa kwenda hata kwenye vijiwe vya kahawa, maana ukifika lazima utaongea tu na ukiongea pengine utaitwa "mchochezi".
Uchochezi ni upi haswa?
. kukosoa yale yanayofanywa na mtu tuliyemchagua kwa kura zetu?
. kuikosoa serikali ambayo sisi ndiyo tuliiweka madarakani?
. kuwaelimisha ndugu zetu ambao hawana fursa ya kupata habari juu ya demokrasia?
Uchochezi ni kitu gani hasa?
 
Back
Top Bottom