Lubebenamawe
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 1,972
- 2,232
Ukweli ni kwamba kuna ukame katika sehemu kubwa ya nchi ambao kwa miezi ya mbele kuna weza kuwepo upungufu mkubwa wa chakula. Hata hivyo ukame wa sasa hauwezi kuwa ndio njaa yenyewe kwa sababu lazima tukubali kwamba mwaka jana karibia sehemu zote nchi walipata mavuno ya kutosha. Kwa takwimu za serikali na wapinzani zinaonyesha kwamba kulikuwa na ziada ya chakula kiasi kwamba wabunge hususan wa upinzani walikuwa wakishinikiza serikali iruhusu wananchi kuuza mazao yao nje ya nchi.
Sasa iwapo chakula kilipatikana cha kutosha kipi kinasababisha njaa inayotangazwa na wapinzani?? Je hata kama mvua ingelikuwa imenyesha kwa kiwango cha kutosha tangu Novemba hadi sasa kuna mkulima angelikuwa ameshavuna mazao yake sasa hivi???
Serikali inatambua kwamba kuna ukame ndio maana inasisitiza wananchi kulima mazao yanayostahimili ukame. Lakini serikali pia ina uhakika kuwa hali ya chakula nchi si mbaya maana kuna chakula cha kutosha.
Serikali ikitangaza njaa kuna madhara makubwa yatatokea ambayo yatamuumiza mwananchi:
a. Kutatokea mfumuko wa bei ambao utanufaisha wafanyabiashara ambao watapandisha bei ya nafaka kwa kigezo cha kwamba kuna njaa.
b. Kuna wafanyabiashara wanaweza kuficha nafaka ili kutengeneza uhaba wa nafaka kwa ajili ya kupandisha bei.
Binafsi nakubaliana na serikali kusisitiza kuwa hali ya chakula ni nzuri kuna nafaka ya kutosha. Kumbukeni nchi hii kuna watu hawana huruma na watanzania wao kutafuta maslahi hata kama ni kwa kuumiza wengine. Tuache ushabiki wa kushabikia watu wanao tafuta maslahi yao.
Naomba kuwasilisha
By Lubebenamawe