Hili ni suala nyeti! Kwa vile lipo basi ni busara lijadiliwe.
Tohara kwa wanawake ilifanywa na makabila ya wafugaji na wawindaji wa kale. Lengo lilikuwa kudhibiti ashki ya muwasho wa kimapenzi ili wasije ipata wakati waume zao ama wako malishoni ama mawindoni.
Enzi hizo kila mwanamke wa makabila hayo alijisikia sifa na heshima kubwa kutahiriwa na asiyetahiriwa alionekana ni mchafu na asiyefaa.
Tohara yenyewe ilitofautiana kati ya kabila na kabila, ila ilihusisha kukatwa kwa clitoris ya mwanamke ambayo ndio the most sensetive part ya female genitalia.
Kutokana na kukatwa sehemu hiyo mapema kabla haijapata mihemuko, sexual sensetivity ta wanawake waliotahiriwa inahamia ndani ya vigina yenyewe na huweza kuamshwa kwa tendo halisi la ndoa na sio kwa kushikwa shikwa tuu kama wasiotahiriwa.
Kimsingi lengo la zamani lilikuwa na nia njema, kwa sasa wakati huo umepita. Hakuna tena wafugaji wanaokaa msimu mzima na malisho ama wawindaji wanaoshinda maporini mwaka mzima.
Kutokana na malengo yaliyohitaji tohara kwa sasa yamepungua ama kutokuwepo kabisa, hakuna sababu ya kuendelea kwa tohara ambacho ni kitendo cha kikatili dhidi ya wanawake. Mkumbuke wanawake wanafanyiwa tohara kwa ajili ya wanaume, kama wanaume wanavyotahiriwa kwa ajili ya wanawake, vita dhidi ya tohara, iwalenge wanaume zaidi.
Ni kama vita dhidi ya biashara haramu ya ukahaba kamwe haiwezi kuisha mpaka atakaporudi Masiya kwa vile wanawake wanaonewa bure, wao wana bidhaa na wanunuzi wapo. Labda ifanywe kampeni ya kuwafanya wanunuzi wasusie bidhaa, wauzaji wakikosa wanunuzi bidhaa zitawadodea na biashara itaisha.
Tena afadhali ya tohara za wanawake wa makabila ya kibantu. Makabila ya Nilotic, yaliyoko Somalia, Sudan, Chadi na Mali, wanawake hao walikatwa kisimi na kushonwa huku wakiachia kitundu kidogo tuu cha kupitishia haja ndogo na hedhi mpaka ukishapata mchumba ndipo njia ifunguliwe tena kwa kisu/wembe. Inakuwa ni mateso mara mbili.
Hapa Tanzania japo tunapiga kelele sana kuhusu mila hii potofu, baadhi kama Wachagga wameiacha kabisa tangu waanze kulima kahawa. Japo wachache wanaiendeleza kwa siri, hawa ni wale ambao wameolewa kijijini, mama anaishi kijijini kazi kukatia ng'ombe majani, na baba anaishi mjini Dasalama, kurudi kijijini
Ni krismasi hadi krismasi. Lakini Wamasai huwaambii kitu. Tena
Wambulu, Wairaqui na Wabarbeig ni sehemu ya maisha yao.
Wanawakata watoto wakike wakishazaiwa tuu ni kukata kitovu na tohara hapo hapo.Msichana anakua wala hajui kuhusu tohara wakiamini wao wamezaliwa hivyo hivyo walivyo.
Madhara ya tohara ni makubwa kuliko hayo ya wanawake wenyewe. Kutokana na mila za tohara, wanaume wa makabila hayo hawajui mapenzi, kwao sex ni kwa ajili ya kutengeneza watoto tuu na sio starehe.
Ndio maana hata leo wanawake wa Kichagga waliokulia kijijini, wanakabiliwa na sexual inhibitions kiasi kwa wengi hata orgasm, hawaijui maisha yao yote. One good thing is,'you can never miss things you have never known'.
Mpaka leo Mmasai humwambii kitu kuhusu tohara. Fanya utafiti utagundua wapinga tohara ni makabila mengine tuu, wamasai wao wamejinyamazia kimyaa. Leo hebu mshauri Edward Lowasa asimame jukwaani awahimize Wamasai waache tohara, mbona atatafuta pa kutokea.
Utafiti wangu ambao sio scientific umegundua baadhi ya wanawake wa makabila ya tohara ambao hawatahiriwa ukigusa tuu, unapata wa urahisi kama mteremko!. Na hawa ndio wengi huwa viruka njia hata katika ndoa zao.
Kama wewe ukifanya sex raha yako ni pamoja na mwenzako kufika, ukipata aliyefanyiwa toara kumfikisha ni ishue unaweza kuishia frustration kwako kushindwa kumridhisha mwenzio kumbe yeye anatoshekea- hapo hapo unapoishia wewe.
Kwa maoni yangu, namna bora zaidi ya kupiga vita ukeketaji ni kuruhusu yale makabila wanaoendeleza tohara, kuifanyia mahospitalini na vituo vya afya chini ya uangalizi wa madaktari ili kuzuia madhara ya matumizi ya vifaa duni na huduma duni zinazochangia vifo vya wakeketwaaji na matatizo wakati wa uzazi.
Hii itaondoa usiri na ndipo kampeni za uelimishaji zifanyike na hatimaye ukeketaji utatokomezwa kabisa.
Kuruhusu ukeketaji kufanyikia hospitali ni mfano hai kwa nchi zilizoruhusu utoaji mimba kisheria na kufanyikia hospitali, kumepunguza sana vifo vya kinamama na idadi ya watoto wa mitaani. Amini usiamini, kila mtoto mmoja anayetupwa kwenye mfuko wa rambo, kuna watoto wengine 9 wametumbukizwa kwenye mashimo ya vyoo vya shimo, ama kutupwa maporini na kuliwa na mbwa maana hadi mfupa wake unatafunika!.
Nchi ya Uswisi imeruhusu matumizi ya madawa yoyote ya kulevya kwa kutenga eneo maalum kwa matumizi hayo. Hili ni eneo la uwanja mkubwa wa wazi mbele ya jengo la bunge la nchi hiyo maarufu kama The Bundes House. Hapa wavuta bangi, wavuta cocaine na wanajidunga heroin wamewekewa manesi wa kuwadunga kwa sindano mpya kila mtu na yake. Wakati huo huo tahudumu wa taasisi za kuzuia matumizi ya madawa hayo zikitoa uelimishaji hatimaye wamefikia kiwango cha watumiaji wanakuja uwanjani hapo kujivutia tuu bangi na kutumia madawa hayo kwa raha zao katika viwango vinavyokubalika. Mpaka sasa madawa yoyote ya kulevya hayana dili Uswisi na badala yake ni dili kubwa Marekani na Uingereza ambako ni marufuku na ni Bonge la dili China na Uarabuni ambako ukishikwa nayo ni kunyoongwa tena bila kutoa taarifa wewe ni raia wa nchi gani.
Tupige vita ukeketaji kwa kuwaelimisha wakeketaji kukubali kuwa ukeketaji ni ukatili dhidi ya wanawake na ndipo wataacha kukeketa, na kuwaelimisha wanaume wao kwamba watafaidi zaidi wanawake wasiokeketwa ili wasiendelee kutafuta wanawake walio keketwa ndipo mila hii itatoweka kabisa na baadhi ya NGO zitafungwa na kutafuta namna nyingine ya ulaji.