Nyendo JF-Expert Member Joined Jun 4, 2017 Posts 1,415 Reaction score 5,014 May 27, 2020 #1 Supu ya nyama. Mahiiaji: Nyama ya mifupa 1/2kg Carrots 2 Viazi 2 Njegere kiasi Kitunguu swaumu 1 tsp Tangawizi mbichi 1 tsp Pilipili manga 1tsp Bizari nyembamba 1tsp Chumvi kiasi Matayarisho: Safisha nyama weka kwenye jiko bila kutia maji. Tia binzari nyembamba, tangawizi, pilipili manga, kitunguu swaumu na chumvi. Pika bila kutia maji igeuze nyama mpaka yote iwe rangi moja, acha kwenye jiko mpaka maji yakauke. Ikishakuwa kavu tia maji ya kutosha kwa ajili ya kuivisha nyama. Acha ichemke mpaka iive vizuri. Kata karoti tia kwenye supu, acha zichemke kwa dakika kama mbili halafu tia njegere na viazi. Viazi vikishaiva onja kama kila kitu kiko sawa. Ukipenda weka na ndimu. Tayari kwa kuliwa. Waweza kula na chapati.
Supu ya nyama. Mahiiaji: Nyama ya mifupa 1/2kg Carrots 2 Viazi 2 Njegere kiasi Kitunguu swaumu 1 tsp Tangawizi mbichi 1 tsp Pilipili manga 1tsp Bizari nyembamba 1tsp Chumvi kiasi Matayarisho: Safisha nyama weka kwenye jiko bila kutia maji. Tia binzari nyembamba, tangawizi, pilipili manga, kitunguu swaumu na chumvi. Pika bila kutia maji igeuze nyama mpaka yote iwe rangi moja, acha kwenye jiko mpaka maji yakauke. Ikishakuwa kavu tia maji ya kutosha kwa ajili ya kuivisha nyama. Acha ichemke mpaka iive vizuri. Kata karoti tia kwenye supu, acha zichemke kwa dakika kama mbili halafu tia njegere na viazi. Viazi vikishaiva onja kama kila kitu kiko sawa. Ukipenda weka na ndimu. Tayari kwa kuliwa. Waweza kula na chapati.
Culture Me JF-Expert Member Joined May 24, 2017 Posts 10,494 Reaction score 21,453 May 27, 2020 #2 Wow! Thanks kwa pishi zuri.
Tetramelyz JF-Expert Member Joined Apr 25, 2014 Posts 4,372 Reaction score 12,479 May 27, 2020 #3 Nikija kuoa... kigezo pekee kitakua ni ajue KUPIKA basii
amu JF-Expert Member Joined Aug 8, 2012 Posts 16,143 Reaction score 31,297 May 30, 2020 #4 Ahsante sana soup nzuri sana.