Super smuggler!

Jaguar

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2011
Posts
3,440
Reaction score
1,029
Siku moja Juan akiwa amebeba mchanga kwa baiskeli,alikamatwa mpakani mwa Mexico na askari wa kuzuia magendo.Wakamwuliza amebeba nini?akajibu;mchanga!.Askari wakaomba kuukagua mzigo,walipocheki ndani ya mfuko,ni kweli ulikuwa mchanga wa kawaida.Ikawa kila mwisho wa wiki lazima Juan apite pale mpakani akiwa na mzigo wake kaupakia kwenye baiskeli,wakimkagua wanaambulia mchanga tu.Siku moja mmoja wa wale askari alimkuta Juan akiwa Bar anapata beer kidogo.Baada ya kumsalimu,yule askari akamwambia Juan;'we mjanja sana,kila siku unapita pale mpakani na baiskeli yako,tukikagua mzigo wako tunaambulia mchanga tu,lazima kuna kitu unavusha ila sisi hatukioni,niambie tu kiurafiki,mwenzetu unavusha nini?'.Juan akacheka kidogo kisha akajibu;'ni kweli,huwa ninavusha baiskeli za wizi kila mwisho wa wiki'!
 
Hahaaa! Nimeipend, Ebwana jamaa anatumia triki ka za osama alivyoishi kwenye kambi ya jeshi
 
ha haaaa haaa.................sasa anavorudi mexico harudi na baiskeli au?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…