Sup sio kilema

Animal Keeper

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
348
282
*SUP SIO KILEMA*


Sup kwangu si kilema,
Ni matokeo ya kitaaluma,
Kama kusoma nilisoma,
Mtihani nikajibu vema,
Moduli zote zilituama,
Imenitokea haijaniuma,
*_Sup Sio Kilema_*
*_Tunasapua Tunasepa_*

Sup ipo *UDOM*,
Mzumbe hadi *SAUT*,
Sup ipo *UDSM*,
Makumira hadi *NIT*,
Sup ipo na *MUM*,
Hadi Mtwara ya *SAUT*,
*_Sup Sio Kilema_*
*_Tunasapua Tunasepa_*

Sup ipo kwa *walimu*,
Madaktari na *mafamasia*,
Sup ipo kwa *mahakimu*,
Hadi wale *mainjiania*,
Wahasibu na *Masikomu*,
Wanasiasa na *wanasheria*,
*_Sup Sio Kilema_*
*_Tunasapua Tunasepa_*

Yawahenga nayakumbuka,
Leo kwangu kesho kwako,
Wewe unayenicheka,
Kesho ni zamu yako,
Usijione umekamilika,
*UE sio mjomba wako*,
*_Sup Sio Kilema_*
*_Tunasapua Tunasepa_*

Tuunde na makundi,
Kwa pamoja tujadili,
Hata sisi hatupendi,
Imetokea kama ajali,
Tulihudhuria vipindi,
Meat na biotechnology,
*_Sup Sio Kilema_*
*_Tunasapua Tunasepa_*

Wapo waajiriwa,
Walisup wakasapua,
Wapo wahemishiwa,
Walisup wakasapua,
Wanasup sije pagawa,
Semista ijayo tutatoboa,
*_Sup Sio Kilema_*
*_Tunasapua Tunasepa_*

Wala usije jificha,
Ukasingizia eti spesho,
Huo uoga jaribu acha,
Ili usisup tena kesho,
Iwe semina iwe lekcha,
Jitahidi kuvuja jasho,
*_Sup Sio Kilema_*
*_Tunasapua Tunasepa_*

*Si kilaza si kipanga*,
Yote amepanga Mungu ,
Tena Sup Sio ujinga,
Nisikilizie Rafiki yangu,
Tena Sup wala si janga,
Nitapata degree yangu,
*_Sup Sio Kilema_*
*_Tunasapua Tunasepa*
1475656745298.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom