Shusha vitu!View attachment 3056224
Part 1:
Ukisoma au kusikia balaa lililomwandama Alexander Litvinenko hadi kifo chake, waweza kudhani ni simulizi kutoka kwenye filamu au riwaya flani...
Huna lolote ni uongo tu unaacha kumalizia storyPart 1:
Ukisoma au kusikia balaa lililomwandama Alexander Litvinenko hadi kifo chake, waweza kudhani ni simulizi kutoka kwenye filamu au riwaya flani. Litvinenko alikuwa shushushu wa shirika la ushushushu la Russia, FSB, katika kitendo cha kubaliana na uhalifu mkubwa (organised crime). Kabla ya kuwa shushushu, Litvinenko alikuwa mwanajeshi ambapo alipanda cheo hadi kufikia ngazi ya ukamanda wa platuni.
Mwaka 1986, Litvinenko alianza kuingia kwenye taaluma ya ushushushu baada ya kuwa 'recruited' kuwa mtoa habari (informant) Shirika la zamani la ushushushu la Russia KGB, katika kitengo cha kupambana na ujasusi (counterintelligence). Miaka miwili baadaye, Litvinenko alihamishiwa rasmi KGB kwenye Kurugenzi Kuu ya Tatu iliyokuwa inahusika na military counterintelligence.
Mwaka huohuo, baada ya kuhudhuria mafunzo ya ushushushu, Litvinenko akawa shushushu kamili katika eneo la kupambana na ujasusi hadi mwaka 1991, ambapo alipandishwa cheo na kuingia katika Federal Counterintelligence Service, shirika la ushushushu baada ya KGB, ambalo lilidumu kutoka mwaka 1991 hadi 1995lilipoundwa upya kuwa shirika la sasa la ushushushu la Russia yaani FSB. Shushushu huyo alipangiwa kitengo kilichohusika na kukabiliana na ugaidi sambamba na kujipenyeza (infiltration) kwenye makundi ya uhalifu mkubwa.
Kadhalika, alikuwa na jukumu la kufuatilia 'maeneo ya moto' (hot spots), yaani maeneo nyeti ndani ya Russia na katika nchi znyingine zilizokuwa ndani ya USSR. Wakati wa vita ya Chechnya, Litvinenko alifanikiwa kupandikiza mashushushu kadhaa ndani ya Chechnya.
Mwaka 1994, Litvitenko alikutana na mmoja wa waliokuwa matajiri wakubwa nchini Russia, Boris Berezovsky alipokuwa anafuatilia jaribio la mauaji dhidi ya tajiri huyo.
Hatimaye akaanza kufanya kazi za pembeni kwa ajili ya Boris, na baadaye akawa msimamizi mkuu wa ulinzi wa kibopa huyo. Ofkoz 'ajira' hiyo ya Litvitenko kwa tajiri huyo ilikuwa sio halali lakini dola iliwavumilia hasa ikizingatiwa kuwa mishahara ya mashushushu kama yeye ilikuwa kiduchu.
Itaendelea
Wale tuliosoma Cuba tunajuwa sababu ya thread hii. britanicca njoo hukukwa hiyo ??
Hawa ma KGB wa zamani ambao kwa Sasa ni FSB,ama ma GRU ama najasusi wengine wa Urusi ni watu hatari sana hapa duniani.Part 3: Mwisho
Novemba 2006, Litvinenko aliugua ghafla na kulazwa. Baadaye, vipimo vilibaini kuwa alidhuriwa kwa kemikali ya sumu ya Radionuclide Polonium-210.
Katika mahojiano, shushushu huyo alieleza kuwa alikutana na mashushushu wawili wa FSB Dmitry Kovtun na Andrei Lugovoi.Japo wote wawili walikanusha kumdhuru shushushu mwenzao, nyaraka zilizovuja za Ubalozi wa Marekani zinaeleza kuwa chembechembe za kemikali iliyomdhuru Litvinenko zilikutwa kwenye gari alilotumia Kovtun huko Ujerumani.
Baadaye mwezi huo, Litvinenko alifariki baada ya moyo wake kushindwa kufanya kazi kutokana na sumu iliyomdhuru. Kabla ya kifo chake, shushushu huyo aliandika taarifa iliyoeleza ameuawa.
Juzi, taarifa ya uchunguzi wa kifo chake ilieleza kuwa njia iliyotumika kumuuwa ilikuwa ni ya hatari zaidi kutokea katika Nchi za Magharibi.
Dokta Nathaniel Cary alieleza kuwa kifo cha shushushu huyo mwili wake ulidhurika vibaya mno kabla ya kifo chake kiasi kwamba ililazimu awekwe katika wodi maalum amapo wagonjwa hutengwa kwa ajili ya uchunguzi wa hali ya juu. Alisema kuwa shushushu huyo aliuawa kwa mionzi ya sumu. Kifo chake kilitokea takriban wiki tatu baada ya kunywa chai ambayo baadaye ilifahamika kuwa ilinyunyiziwa sumu ya Polonium.
Dokta Cary alieleza kuwa yye na timu yake walilazimika kuvaa suti mbili za kujikinga (kama zile za matabibu wa Ebola) ambazo ziliwekwa hewa ndanikupitia mirija maalum ili kukwepa athari za sumu husika. Alisema, "uchunguzi huo wa maiti ulikuwa ni usio wa kawaida kabisa katika historia ya nchi za Magharibi".
Mwisho
Mimi tena mkuu???🤣🤣😂Malizia basi kipande kilichobakia