Sumaye: Zanzibar kina kirefu kwa Magufuli

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,701
71,035
Wakuu habari za asubuhi,

Waziri mkuu Mstaafu mh. Fredrick Sumaye amesema mgogoro unaoendelea Zanzibar ni kina kirefu kwa Magufuli.

Chanzo: Mtanzania
 
Nguvu anayo sana tu, sema hataki kusimamia maamuzi ya wazanzibari bali anataka kukibeba chama chake
Mkuu kwa jinsi ninavyoelewa tatizo la Zanzibar si la kiusalama bali ni la kisiasa sasa Rais wa JMT anaingia vipi? Na kwa mfumo wa Muungano tuna Zanzibar na Tanzania hatuna Tanganyika na tunachanganywa mara Zanzibar ni nchi mara sio nchi(ila ina Rais na serikali kabisa) hivyo Rais wa JMT ni kama mshauri kwenye mambo ya kisiasa upande wa Nchi jirani
 
Mkuu tatizo la zanzibar ni shein kupora ushindi wa maalim Seif Sharif Hamadi, hii ni dhuluma kwa wazanzibari kwa hiyo anachotakiwa kufanya magufuli ni kusimamia haki tu basi
 
Watu wanasahau kuwa tatizo la Zanzibar halikuanza jana wala juzi. Magufuli amezungukwa na washauri wakiwemo marais wote wastaafu. Uamuzi wake kuhusiana na issues zozote zile hata siku moja hauwezi kuwa ni wake binafsi bali ni uamuzi wa taasisi inayoitwa urais.
 
Kwa hiyo tunatarajia uamuzi wowote ule utakuwa katika misingi ya haki
 
binafsi;-
zipo nguvu mbili hapa/
1/ chama/aka ccm
2/ RAIS.
mtazamo wangu binafsi,RAIS magufuli hana Tatizo,tatizo chama/ aka ccm / na wahafidhina wake!/ ona hata ktk umeya tu ni tatizo!!!
*watu hawa nawafananisha na vile vizee vilivyopo klabu ya yanga,/havitaki kwa kufa au kupona yanga Kampuni /ati vitakosa ulaji!!/ vimeshajizoelea !!
 
sumaye nadhani amemuelewa magufuli kuwa dhamira yake ipo kwenye haki kwamba kufuta matokeo majimbo yote haikuwa fair. mtazamo wangu ni kuwa magufuli na membe wanaweza kuwa team moja kwenye hili. membe yeye alisema kwenye vyombo vya habari ya kwamba haikuwa sahihi kufuta matokeo majimbo yote.
 
Huwezi ukamwambia mwenzako aachie kiti wakati mbinu zile zile zilizofeli kwa mwenzako ndio wewe zilikufanikisha kuingia madarakani sasa hapo ukijitoa ufahamu ndio kutatokea mwaga mboga nimwage ugali
 
Back
Top Bottom