SUMAYE: Wizi wa kura utatuponza

SUMAYE: Wizi wa kura utatuponza

nashangaa kumbe kuna watu bado wanamsikiliza huyo mr. zero. sifuri ni sifuri tu hata uzidishe au ugawanye na herufi.
 
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, amesema wizi wa kura na uchakachuaji wa matokeo ya chaguzi, ni miongoni mwa vitu vinavyosababisha vurugu na kufifisha amani kwa nchi na watu wake.

Sumaye aliyasema hayo wakati akihutubia mkutano mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, uliofanyika jana jijini Arusha. Ujumbe wake ulijikita katika uwapo wa umoja, amani na utulivu.

Pamoja na mambo mengine, Sumaye alitumia hafla hiyo kumpongeza, Askofu Mteule, Mchungaji Solomon Massangwa, kwa kuchaguliwa kuiongoza dayosisi hiyo kujaza nafasi iliyoachwa wazi kutokana na kifo cha Askofu Thomas Laiser.

Akizungumzia vurugu zinazohusiana na masuala ya siasa, Sumaye alisema uvunjifu wa amani unatokea pale upande mmoja unapohisi kudhulumiwa au kuonewa katika maamuzi ya kisiasa hasa nyakati za kampeni, upigaji kura na wizi wa kura.

“Wakati mwingine hali hii hutokea kwa upande moja kukataa kushindwa hata kama wameshindwa kwa halali.

Jambo hili la kisiasa limeleta fujo nyingi hasa katika nchi nyingi za Kiafrika na kusababisha umwagaji wa damu,” alisema.

“Ni lazima shughuli zetu za siasa zifuate sheria na taratibu zilizowekwa kwa uwazi bila kutiliwa shaka na upande wowote. Haki ni lazima isimamiwe kikamilifu nyakati zote za kampeni hadi upigaji wa kura, kuhesabu kura na hata kutangaza matokeo,” alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, Tanzania inahitaji kuendeleza umoja miongoni mwa raia wake, ili kuimarisha utulivu na kuvunja migawanyiko nchini.

Kwa mujibu wa Sumaye, nchi zenye uvunjivu wa amani kiasi cha kuwapo vita vya wenyewe kwa wenyewe, zimefikia hali hiyo kutokana na kuwapo kundi linaloamini kudhulumiwa haki zao na wakati mwingine ni kutokana na chuki iliyojengeka kati yao.

UDINI
Sumaye alisema chuki zinazoelekezwa kwenye imani za kidini zinapaswa kukemewa kutokana kuwa na madhara yanayoiathiri jamii nzima.

Alisema hivi sasa kuna chokochoko zenye sura ya imani zinazochangia kufifisha upendo na uzalendo, hivyo kuathiri umoja uliopo.

“Tukiwa wamoja hili halina nafasi kwa sababu hakuna dini inayofundisha chuki kwa binadamu mwenzake,” alisema.

Alisema viongozi wa dini wanapaswa kuwasimamia waumini wao, ili nchi isije ikakumbwa na balaa la vurugu za kidini, jambo ambalo ni la hatari na lisilopaswa kutokea.

TOFAUTI ZA KIPATO
Sumaye alikemea pia kushamiri kwa tofauti kubwa ya kipato baina ya makundi tofauti, hasa kati ya matajiri wachache na wenye madaraka kwa upande mmoja na maskini walio wengi kwa upande wa pili.

Alisema tofauti hizo zinasababishwa na mfumo mbaya wa uchumi na ubinafsi uliokithiri ama usiojali binadamu wengine.

“Hali hii ni ya hatari kwa amani na utulivu kwa sababu walio wengi hawatavumilia kuwaona wachache wakiishi katika anasa za kutisha wakati wao hawamudu hata mahitaji ya lazima kama vile chakula, matibabu na maji,” alisema.

Alisema hali kama hiyo imesababisha vurugu katika nchi nyingi na kuathiri amani na utulivu na kwamba hata hapa nchini, kuna tofauti kubwa ya kipato kwa makundi hayo hivyo inahitajika kudhibitiwa kwa haraka.

Sumaye alisema kutokana na hali hiyo, ipo haja ya kuwekeza na kutekeleza mipango inayochochea uzalendo wa kuipenda nchi na watu wake.

Waziri Mkuu mstaafu huyo, alisema kukosekana kwa umoja ni miongoni mwa sababu zilizofifisha maendeleo katika nchi nyingi za Bara la Afrika.

VIONGOZI WA DINI
Alisema viongozi wa dini wana kazi kubwa katika wakati huu kuliko ilivyokuwa zaidi ya muongo uliopita.

Alisema ukosefu wa maadili umekuwa chanzo cha kuibuka kwa matatizo kadhaa ya kijamii na kuhoji, “Je, katika upungufu huu wa maadili, viongozi wa kiroho mna nafasi ipi ya kudhibiti mambo haya?”

Sumaye alisema viongozi wa serikali, dini na asasi nyingine za kijamii wana jukumu la kuuongoza umma, badala ya kuliacha (jukumu hilo) kwa kikundi kimoja.

AMANI KWA MAKANISA
Alisema umoja unatakiwa kuwapo hata kwenye madhehebu ya dini, ambako waumini wanatakiwa kumheshimu na kumtii kiongozi anayechaguliwa.

“Kama hamtakuwa na umoja maana yake hapatakuwa na upendo baina yenu, amani na utulivu vitaathirika na hatimaye maendeleo ya kimwili na ya kiroho yatakuwa ni ndoto za alinacha,” alisema.

Aliongeza: “Siku hizi hutokezea hata katika chaguzi za nafasi za uongozi makanisani watu kujitenga na viongozi waliochaguliwa eti kwa sababu tu huyo aliyechaguliwa hakuwa chaguo lake, hali ambayo huwafanya viongozi kuongoza kwa shida sana.”


Source:
NIPASHE.

Kanisa limekua chaka la wasaka tonge la kisiasa
 
Heri yeye aliyejitambua kuliko hao interahamwe wenzake wasiowaza zaidi ya urefu wa pua zao!

CCM kuna changamoto za kawaida, CDM kuna shida zisizoisha! Ni mpango wa shetani kupata kundi la watu ndani ya nchi ambao kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 6 usiku ni kulaumu tu basi. Hali kama hii ilitokea kwa MUNGU ambapo shetani na Lusifa ndizo zilikuwa tabia zao! CDM - USHETANI - LAANA!
 
Heri yeye aliyejitambua kuliko hao interahamwe wenzake wasiowaza zaidi ya urefu wa pua zao!

Naunga mkono hoja. Naona sasa huyu anafaa zaidi ya walidhani ikulu ni mahali pa kufanyia biashara. Wanaopigana vikumbo sijasikia wanaonaje hali ya watanzania. Umaskini wa watanzania walio wengi sijasikia ukizungumzwa na viongozi waliopo madarakani wala wanye nia ya kugombea urais nimemsikia huyu sasa. Nadhani anayo mission ya kusikulizwa kuliko hao wengine wanaotaka kwenda kuifanya ikulu pango la wanyang'anyi.
 
Tangu nimeanza kuchangia leo ndo nimeona Lizaboni na mwanadiwani wakikimbia huu uzi mko wapi njooni jamani tukate utepe! Go go go SUMAYE
 
Mhhh!! Yamekuwa mang'ana tata! Eeheeee! Laana ya kunga'ang'ana na serikali mbili ndo hiyo. Watu wanaanza kutoa hasira zao.
 
Tusipo rudisha rasimu ya Warioba kwenye mstari tutapasuka wengi sana.
 
Sumaye usitishwe na mawakala na vibaraka wa ufisadi wanaotaka uongozi kwa kununua wapiga kura kaza buti sema usichoke wapo watu mamilioni tunaokuunga mkono.Kama Sumaye anakemea rushwa halafu mtu anatukana basi huyo mtu anatumiwa.Kiongozi yeyote anaye kemea maovu anapaswa kuungwa mkono ili kuninusuru Taifa letu dhidi ya uovu huu mbaya wa rushwa wakati wa uchaguzi.
 
Nafikiri Mh Sumaye angekaa kimya afanye shughuli zake ili ajiletee maendeleo zaidi kwani matamshi yake yanatia kichefuchefu. Mtu aliyekaa madarakani kwa miaka kumi na ktk kipindi hicho chaguzi nyingi ndogondogo na kubwa zimepita na chama chake kikishinda chaguzi nyingi, ivi hakujua ushindi ule ulitokana na wizi wa kura? Kwa nn asiseme na aseme leo? Mzee Sumaye, kwa viwango vya sasa umeshazeeka ki-elimu na ki-umri pumzika kama mwenzako Mzee Cleopa Msuya(CD). Tz ni maskini lkn ww hujui kwa nn ni maskin, uliutangazia ulimwengu ulipokuwa Marekani - ni mtihani

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Sumaye usitishwe na mawakala na vibaraka wa ufisadi wanaotaka uongozi kwa kununua wapiga kura kaza buti sema usichoke wapo watu mamilioni tunaokuunga mkono.Kama Sumaye anakemea rushwa halafu mtu anatukana basi huyo mtu anatumiwa.Kiongozi yeyote anaye kemea maovu anapaswa kuungwa mkono ili kuninusuru Taifa letu dhidi ya uovu huu mbaya wa rushwa wakati wa uchaguzi.

Na hiyo rushwa kaiona leo wakati yuko saa 11? Wakati akiwa waziri mkuu hiyo rushwa haikuwepo? Alisikika lini wakati wa uwaziri mkuu wake akikemea vitendo vya rushwa na ufisadi?Hiyo hatari kubwa anayoiona kati ya walio nacho na wasio nacho haikuwepo au kuonekana na kukemewa enzi za uwaziri mkuu wake? Nini kinacho mwaminisha kuwa wananchi kwa sasa watamuona ni bora kuliko awali?Asichokielewa ni kuwa watanzania wale wale waliokuwa wakiwachukulia kutokuwa na uelewa wa masuala ya siasa sasa hivi ni waelewa kuliko wengi wa wanasiasa mliopo.
 
Back
Top Bottom