comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha demokrasia na maendeleo ambaye pia ni Waziri mkuu mstaafu Mh Frederick Sumaye amesema kwamba serikali inayoongozwa na Rais Magufuli chini ya chama cha mapinduzi CCM ilitoa ahadi ya kuinua na kuboresha maisha ya watanzania badala yake imeyadidimiza na kuzidisha ugumu wa maisha ya watanzania ,Mh Sumaye amesema lengo ni kuitoa madarakani serikali inayoongozwa na ccm maana imeshindwa kutekeleza ahadi zake zake badala yake imezidisha ugumu wa maisha kwa watanzania.
Chanzo: Tanzania Daima