tajirijasiri
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 2,863
- 3,854
Ukawa kuwapokea Lowassa na Sumaye hawajakosea hata kidogo. Tujikumbushe kidogo juu ya historia ya maendeleo. Najua sio rahisi kwa binadamu kuwa msafi kwa 100%, hasa unapokuwa kwenye Mfumo fisadi wa CCM. Lakini kipindi cha viongozi hawa wawili ndicho kipindi pekee ambacho Serikali ya Tanzania angalau iliweza kufanya maamuzi muhimu yenye manufaa kwa watu.
Sumaye: Akiwa Waziri Mkuu aliwezesha Serikali ya Awamu ya Tatu kudhibiti mfumko wa bei ambao unagusa moja kwa moja maisha ya watu.
Lowassa. Akiwa Waziri Mkuu, alisimamia kwa dhati uanzishwaji wa Shule za kata ambazo kwa kiasi kikubwa zilisaidia kuwakomboa kielimu watoto wa maskini ambao hapo awali walikosa nafasi ya kuendelea na elimu ya Sekondari.
Haya ni baadhi ya mambo ya msingi. Yapo mengi wengine mtaongezea.
Najua walifanya makosa, kwani wao si malaika. Lakini makosa hayo yalichangiwa sana na mfumo fisadi wa CCM. Kwa vile wamuamua sasa kuachana na mfumo huo fisadi, basi Ukawa wako sahihi kuwapokea ili waongeze nguvu kusaidia kuiondoa CCM.
Ukawa shikamaneni daima mpaka kieleweke.