Sumaye: MV Bukoba ilikuwa na ‘mkono wa mtu’

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, amesema ajali ya meli ya MV Bukoba iliyotokea mkoani Mwanza takribani miaka 20 iliyopita haikutokana na mapenzi ya Mungu bali ni uzembe uliosababishwa na makosa ya binadamu.

Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu ya kumbukumbu ya miaka 20 tangu kutokea kwa ajali hiyo; Mei 21, 1996, Sumaye alisema mojawapo ya matatizo makubwa

yanayosababisha ajali zisiishe nchini ni watu kukubali kila kitu kuwa ni “Matakwa ya Mungu”.
Katika mahojiano hayo ambayo yamechapwa yote katika gazeti hili kwenye kurasa za kati, Sumaye alisema kilichosababisha ajali ya MV Bukoba kilikuwa ni kujaza abiria na mizigo mingi kwenye meli – kinyume cha uwezo wa meli hiyo na kwamba huwezi kusema kwamba ajali ile ilitokana na mapenzi ya Mungu.

“Wengine wanasema ajali ni mipango ya Mungu lakini sikubaliani kwa sababu ajali ya MV Bukoba haikuwa ni tatizo la kiufundi, ilitokana na makosa ya kibinadamu kutokana na meli kujaza abiria na mizigo zaidi ya uwezo wake. Kwahiyo ilipokuwa ziwani ikakumbana na upepo mkali na hivyo kutokana na uzito uliokuwa umezidi, basi meli ikapinduka.

“Ajali hata za barabarani zina mkono wa binadamu kutokana na uzembe kama ulevi, mwendo kasi na mengineyo na ajali zinaepukika kama wahusika watachukua tahadhari za usalama wa chombo husika, “ alisema Sumaye ambaye ndiye Waziri Mkuu aliyekaa madarakani kwa muda mrefu kuliko mwingine yeyote katika historia ya Tanzania.

Sumaye alitumia fursa hiyo kueleza kuwa mojawapo ya namna ya kupunguza ajali zinazoua maelfu ya wananchi kila mwaka ni kuhakikisha wamiliki wa vyombo vya usafiri wanawalipa marehemu na majeruhi; stahiki zao halali za bima tofauti na ilivyo sasa ambapo watu wanapata ajali na hawafidiwi kwa vyovyote.

“Ndiyo kuna mengi sana ya kujifunza kutoka katika ajali ile kuanzia zoezi la uokoaji hadi ulipaji wa fidia kwa watu waliopoteza maisha na wale waliojeruhiwa –kwamba mfumo wetu wa kulipa fidia bado hauko sawa. Kwamba serikali haina uwezo mkubwa wa kifedha wa kulipa wahanga wa ajali na tatizo hilo lipo hadi leo.

“Nakumbuka kwa wakati ule serikali ilitoa kifuta machozi cha shilingi 500,000 kwa watu waliopoteza maisha na shilingi 100,000 kwa waliojeruhiwa na kiasi hicho kwa kweli kilikuwa kidogo sana lakini hatukuwa na jinsi kwa sababu serikali haikuwa na fedha za kutosha.

Hata makampuni ya usafirishaji wa majini na nchi kavu hayajaweka utaratibu wa kuwalipa fidia kwa kutumia bima pale abiria au mteja wao anapopata ajali na chombo husika. Nadhani kuna haja ya suala hilo kufanyiwa kazi ili basi abiria anapopata ajali basi haki zake zizingatiwe kwa kulipwa fidia kupitia bima na kampuni husika ihakikishe kila wakati wanakuwa na bima itakayozingatia maslahi ya mteja wao,” alisema Sumaye.

Katika mahojiano hayo yaliyofanyika jijini Arusha, Sumaye ambaye alikihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana, alisema hawezi kusahau ajali ile kwa sababu ilihusu maisha ya watu wengi.

Alisema kama Waziri Mkuu, alikuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa janga lile la kitaifa linashughulikiwa ipasavyo; ikiwamo kuomba msaada katika nchi rafiki katika masuala ambayo yalikuwa kinyume na uwezo wa serikali ya Tanzania wakati huo.

“Kipindi cha janga ni katika vipindi vigumu unapokuwa kiongozi mwenye wajibu wa kusimamia zoezi la uokoaji. Kwa mfano, mimi katika kipindi hicho kuna wakati nilikuwa nakesha usiku kucha kuongoza vikao vya kamati ya maafa kuongoza kamati ya ukoaji na kuzungumza na wadau mbalimbali.

“Ni kipindi ambacho kuna wakati unasahau hata kula chakula kutokana na ratiba ya kazi kuwa ngumu na isiyotoa fursa kwa muda kupotea kwa sababu unashughulika na uhai na maisha ya watu. Pamoja na ajali ya MV Bukoba, katika kipindi changu nakumbuka nimeratibu mazishi ya Baba wa Taifam Mwalimu Julius Nyerere, na janga la ajali ya treni mkoani Dodoma ambayo pia iliua zaidi ya watu 200,” alisema Sumaye. -

Raia Mwema

=======================================
Maoni yangu

Sumaye anaposema "makampuni ya usafirishaji wa majini na nchi kavu hayajaweka utaratibu wa kuwalipa fidia kwa kutumia bima pale abiria au mteja wao anapopata ajali na chombo husika.

Pili anaposema haja ya suala hilo kufanyiwa kazi ili basi abiria anapopata ajali basi haki zake zizingatiwe kwa kulipwa fidia kupitia bima na kampuni husika ihakikishe kila wakati wanakuwa na bima itakayozingatia maslahi ya mteja wao

Kwanini Sumaye hakuyafanya haya wakati yalikuwa ndani ya uwezo wake wakati akiwa waziri mkuu kwa miaka kumi au ndio njia ya kua kutulaghai na kutufanyia isitidhai?

Tatu kwa kukiri kwake kuwa ajali ya MV bukoba ilikuwa ni uzembe na kweli ni uzembe baada ya srikali kushindwa mpaka kesi mahakamani, kwanini hakujiuzulu kwa serikali aliyokuwa anaisimamia kusababisha watanzania zaidi ya 1000 kupoteza maisha kwa uzembe kama anavyokiri mwenyewe?
 
Inasikitisha kusikia haya maneno toka kwa PM mstaafu, especially kama haya yote yalitokea "under his watch"
 
pumba tupu

swissme
 
alipokuwa waziri mkuu angechukua hatua...yeye aliendekeza ufisadi tu na kujilimbikizia mali...sumaye ndio mmiliki wa mount meru hotel ya arusha
 
Huyo mzee ni tajiri sana, ana mashamba makubwa makubwa, yaani hata PM mstaafu Mizengo Pinda ni maskini sana kwa Sumaye.
 
alipokuwa waziri mkuu angechukua hatua...yeye aliendekeza ufisadi tu na kujilimbikizia mali...sumaye ndio mmiliki wa mount meru hotel ya arusha
Sasa tatizo liko wapi kama umiliki wake ni wa halali.vigogo wengi wanamiliki mahotel mkuu
 
Nilisema humu kwamba katika kununua meli mpya for Lake Victoria, Serikali isirudie makosa ya MV. Bukoba. Wajenge modern shipyard pale Mwanza ili meli zijengwe hapohapo, badala ya kuleta meli toka Ulaya na kuisafirisha kwa treni au Barbara toka banadarini Dar hadi Mwanza; kwani kufanya hivyo ilibidi MV. Bukoba ikatwe vipande kadha ili kufiti katika magari maalum yaliyovisafirisha kwa barabara hadi Mwanza; ambako vipande hivyo vikaunganishwa tena.
Kwa uelewa wangu mdogo, na niko radhi kusahihishwa; ni kwamba kutokana na kukatwakatwa na kuungwa upya inasemekana kwamba Mv. Bukoba ilipata ubobu/matatizo ya kimaumbile ambayo sitayataja hapa, ambayo yalivuruga utaratibu wa ukaguzi wa chombo kabla ya kupata vibali vya mamlaka za usafiri wa maji na bima. Kwa kifupi nakubaliana na Mh. F. Sumaye kwamba ajali ya MV. Bukoba ilisababishwa na uzembe wa watu wengi, kuanzia juu serikalini mpaka chini kwa waendeshaji. Kwa kumalizia: bora waamue hiyo meli ijengwe Kisumu, Kenya ambako ilijengwa MV. Victoria, halafu iletwe Mwanza, kuliko kurudia makosa niliyotaja hapa juu. Vivyo hivyo kwa Kigoma, ile meli ya sasa Wajerumani waliijenga hapohapo Kg. Hata mambo yanahitaji utaalamu, sio porojo za siasa. Serikali ijifunze kuepuka ahadi bila mipango ya kiufundi na zisizotekelezeka.
 
Mv DAR ilifanya safari moja tu tena ilikuwa inaenda mwendo wa kobe watu wakapiga Bilioni 8....Tumeibiwa KWERI KWERI.
 
Back
Top Bottom