Sumaye hajawahi kuwa mwanachama wa CHADEMA, inakuwaje Mbowe amemteua kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu?

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
49,681
39,015
Wanaukumbi.

.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu wanachama na wafuasi wa Chadema naona sasa hivi hawajuhi hatima yao ndani ya Chadema, imefikia wakati wanasema pembeni kwa hofu ya kufukuzwa chama kama watahoji haya yanayotokea ndani ya chama chao.

Sumaye hajawahi kuwa Mwanachama wa CHADEMA lakini leo hii Mbowe anatutangazia wana Chadema kuwa amemteua kuwa Mjumbe wa Kamati inakuaje Mjumbe wa Kamati Kuu wakati siyo mwanachama wa Chadema? Wanahoji wanachama wa Chadema ambao wameniomba niwasaidie kuwatangazia Watanzania kwa hofu wakijulikana watafukuzwa.

Wanauliza lini Sumaye kajiunga na Chadema na kadi yake ni namba ngapi na kakabidhiwa wapi wanahoji wafuasi wa Chadema kwenye soko la Mwanjelwa Mbeya.

Lowassa pia anaitwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu lakini hakuna uthibitisho wowote kuwa aliwahi kuteuliwa na chama kwenye nafasi hiyo ni maamuzi ya Mbowe akihamua kitu hamna wa kupinga wala kuhoji.
 
Hakuna Shida Maalim Ritz, Lowassa aliteuliwa kuwa Mgombea Urais Chadema 2015 akiwa bado na Kadi hai ya Chama cha Mapinduzi. alijiunga baada ya mazungumzo na Makubaliano kukamilika.
 
Hapana, hoja yako haina ukweli au hujawa updated!

Sumaye ni mwanachama hai wa CHADEMA.

Pitia kwenye hii habari kutoka IPP Media;

Sumaye alikabidhiwa kadi na Mbowe siku ya mwisho wa kampeni za uchaguzi wa Jimbo la Arusha Mjini. Kumbuka uchaguzi wa Jimbo la Arusha ulisogezwa mbele baada ya kutokea kifo cha mgombea wa ACT-Wazalendo, Estomih Mallah.
 
Mkiambiwa Kitwanga zinawaribu mnaka Kwenye Kampeni za uchaguzi wa Ubunge kule Arusha Sumaye Alikabidhiwa kadi pole sana wacheni viroba alafu mnakimbilia huku
 
Hivi ni Kwanini Kila Mara C.C.M Wanapo Banwa Kwenye Kona Kisiasa Huishia Kuitaja taja CHADEMA?
 
Kwa faida ya JF unaweza kutufahamisha nani alimkabidhi kadi ya Chadema Sumaye?
Aliyemkabidhi kadi ni mmiliki wa CHADEMA, Mbowe.

Kumbuka pia Katiba ya CHADEMA inampa madaraka Mbowe kuteuwa watu sita kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.
 
Kwa faida ya JF unaweza kutufahamisha nani alimkabidhi kadi ya Chadema Sumaye?
ALIKABIDHIWA CARD YA CHADEMA NA MWENYEKITI WA CHAMA FREEMAN MBOWE ARUSHA KWENYE KAMPENI ZA UBUNGE WA ARUSHA MJINI NA KAMANDA GODBLESS J LEMA KUIBUKA MSHINDI... INACHOMA LAKINI HUU MCHEZO HAUITAJI HASIRA
 
Mkuu. Ahsante kwa kuthibitisha kuwa Lowasa na Sumaye ni wanachama wa CCM.
Alimaanisha hao wanaosema wanachama wa CHADEMA kutoka Mbeya waliolalamika kwa ritz moko ndio wanachama wa CCM na siyo Sumaye na Lowassa!
Ina maana hapo Lumumba hata vitu vidogo kama hivi mnashindwa kuelewa?
 
ALIKABIDHIWA CARD YA CHADEMA NA MWENYEKITI WA CHAMA FREEMAN MBOWE ARUSHA KWENYE KAMPENI ZA UBUNGE WA ARUSHA MJINI NA KAMANDA GODBLESS J LEMA KUIBUKA MSHINDI... INACHOMA LAKINI HUU MCHEZO HAUITAJI HASIRA
Maelezo yako yanathibitishwa na chanzo kipi cha habari?
 
Alimaanisha hao wanaosema wanachama wa CHADEMA kutoka Mbeya waliolalamika kwa ritz moko ndio wanachama wa CCM na siyo Sumaye na Lowassa!
Ina maana hapo Lumumba hata vitu vidogo kama hivi mnashindwa kuelewa?
Mkuu, mbona unamsemea mtu ilhali mwenyewe yupo?
 
Aliyemkabidhi kadi ni mmiliki wa CHADEMA, Mbowe.
Kamanda weka basi picha ya Sumaye akikabidhiwa kadi ya Chadema kama hii.
2016-05-29-17-24-56-820954749.jpeg
 
Mbona alishakabidhiwa kadi ya uanachama na mambo yalikuwa hadharani?

Pole kwa kukurupuka!
 
Back
Top Bottom